Kila wiki Kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuia magonjwa barani Afrika yaani Africa CDC huangazia maeneo ya afya yaliyopea kipaumbele barani.
Ambapo wiki hii kituo hicho kimeachia taarufa kuhusu hali ya magonjwa vamizi mbalimbali kama vile Marburg, Lassa na Uviko 19.
Je, Africa CDC imeangazia nini wiki hii ?
Kufikia sasa nchi 14 za Afrika zimechanja asilimia 70 ya watu wanaowalenga dhidi ya COVID-19. Hizi ni pamoja na Rwanda, Somalia, Botswana, na Morocco
Katika wiki iliyopita hakuna kisa kipya au vifo vya ugonjwa wa virusi vya marburg vimeripotiwa kutoka Tanzania
Nchini Equitorial Guinea ,Visa 5 mpya vya marburg viliripotiwa
Nchi 10 za Afrika zinaripoti visa vya Kipindupindu. ni pamoja na Kenya, Malawi, Nigerai, Afrika Kusini na Sudan Kusini
Visa vipya19 na vifo 26 kutoka kwa Mpox vimeripotiwa katika Jamhuri ya Afrika ya kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ghana Liberia na Nigeria
Kesi 12 mpya zilizothibitishwa na vifo 3 vipya vya homa ya Lassa vimeripotiwa nchini Nigeria













