| Swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
Kwa Picha: Watu 45,000  waungana katika mbio za kila mwaka Ethiopia
Jumapili mitaa ya mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa ilijaa na msisimko wa hafla ya "Great Ethiopian Run"  mbio za kilomita 10 ya halaiki ambazo hufanyika kila mwaka
Kwa Picha: Watu 45,000  waungana katika mbio za kila mwaka Ethiopia
Watu 45,000 walijisajili kwa mbio za Great Ethiopian Run mwaka huu / Picha kutoka Great Ethiopian Run / Others

Kampuni ya Great Ethiopian Run inasema, zaidi ya wakimbiaji 45,000 walijisajili kushiriki katika mbio za Great Ethiopian Run, jijini Addis Ababa nchini Ethiopia. Mbio hizo zinavutia watu kutoka Ethiopia, Afrika na duniani kote.

Mbio za mwaka huu ziliadhimisha miaka 23 ya hafla hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2001 na mwanariadha mashuhuri wa Ethiopia - Haile Gebrselassie ili kukuza kukimbia kama shughuli ya kiafya.

Kila mwaka idadi ya wanaohudhuria inaongezeka, wengi wakija kwa ajili ya kufurahia na familia na marafiki zao.

Watu wengine hukimbia na wengine kutembea tu lakini kila mtu hupata medali.

Mbio hizo ni zaidi ya mbio tu; ni sherehe ya utamaduni wa umoja wa Ethiopia. Imekuwa ikichangia sana katika kudumisha na kukuza amani na umoja miongoni mwa Waethiopia.

Kila mwaka wanariadha wa kulipwa wenye ulemavu hukaribishwa kuhusika katika kitengo chao maalum za mbio hizo.

CHANZO:TRT Afrika