MICHEZO
2 DK KUSOMA
Paris Olimpiki 2024: Matumaini ya Tanzania kutwaa medali sasa  yabakia kwa wanawake
Hii ni baada ya Alphonce Felix Simbu kumaliza katika nafasi ya 17, huku Gabriel Gerald Geay akishindwa kumaliza mbio za kilomita 42, kwa upande wa wanaume.
Paris Olimpiki 2024: Matumaini ya Tanzania kutwaa medali sasa  yabakia kwa wanawake
Alphonce Felix Simbu( wa Tanzania wanne nyuma) akichuana katika mbio za kilomita 42 kwa upande wa wanaume, jijini Paris siku ya Agosti 10./Picha: Athletics Tanzania / Others
10 Agosti 2024

Macho na masikio ya Watanzania sasa yapo kwa Magdalena Shauri na Jackline Sakilu kwenye michezo Paris Olimpiki 2024, itakayomalizika Agosti 11, 2024 jijini Paris, nchini Ufaransa.

Hii ni baada ya Alphonce Felix Simbu kumaliza katika nafasi ya 17, huku Gabriel Gerald Geay akishindwa kumaliza mbio za kilomita 42, kwa upande wa wanaume.

Wakati Simbu alimaliza katika nafasi ya 17 katika mbio zilizofanyika Agosti 10, kutumia muda wa saa mbili na dakika kumi na sekunde tatu (2:10:03), Geay alishindwa kabisa kumaliza mbio hizo ambazoTamirat Tola kutoka Ethiopia aliibuka mshindi kwa muda wa saa mbili, dakika sita na sekunde tatu (2:06:26).

Licha ya kupeleka timu ya wanariadha katika makala za mashindano hayo makubwa ulimwenguni, Tanzania imeshinda kufanya vizuri kwenye michezo ya Olimpiki.

Ikumbukwe kuwa wanariadha wa zamani Filbert Bayi na mwenzake Suleiman Nyambui, ndio waliofanikiwa kuiletea Tanzania medali kwenye mashindano hayo, wakifanya hivyo kwenye michezo ya Olimpiki iliyofanyika jijini Moscow, Urusi mwaka 1980.

Katika makala ya michezo ya Olimpiki ya jijini Moscow iliyofanyika mwaka 1980, Bayi alimaliza mbio hizo za mita 3000 na kutunukiwa medali ya fedha.

Kwa upande wake, Nyambui pia alishinda medali ya fedha kwenye mashindano hayo katika mita 5000.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika