"Ilitokea kwamba Cyrus Jirongo mwenye umri wa miaka 64 alikuwa akiendesha gari aina ya Mercedes Benz kutoka upande wa Nakuru kuelekea Nairobi na alipofika eneo la ajali, alishindwa kudhibiti njia yake na kugongana uso kwa uso na gari lililokuwa likija," ripoti ya polisi inasema.
Magari yote mawili yaliharibika, huku sehemu ya mbele ya gari la Jirongo ikikumbwa na uharibifu mkubwa zaidi. Picha kutoka eneo la tukio zinaonyesha sehemu ya injini ya sedan ya kifahari ikiwa imeharibiwa kabisa na vifusi vilivyotapakaa kando ya barabara.
Hakuna abiria aliyekuwemo ndani ya basi hilo aliyepata majeraha ya kutishia maisha, ingawa wengi walitibiwa kutokana na mshtuko na michubuko midogo.
Mwili huo baadaye ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha eneo hilo huku wanafamilia na washirika wa karibu walikusanyika Naivasha kwa mipango ya kuhamisha mwili huo hadi Nairobi.
Rais amuomboleza Jirongo
Rais wa Kenya William Ruto ameungana na Wakenya kuomboleza kifo cha Cyrus Jirongo.
‘‘Nimehuzunishwa sana na kifo cha rafiki yangu, aliyekuwa mbunge wa Lugari Cyrus Jirongo,’’ aliandika Rais Ruto katika mtandao wa X. ‘‘ Jirongo alikuwa mtafuta-harakati asiyechoka, mfanyabiashara mwenye uzoefu, na mwanasiasa mkamilifu ambaye alikataa kufafanuliwa, sembuse kushindwa, na changamoto za maisha,’’ alionmgeza Rais Ruto.
Mwingine aliyetuma rambirambi kwa familia ya Jirongo ni Francis Atwoli, katibu mkuu wa muungano wa wafanyakazi COTU.
‘‘Asubuhi ya leo, nikiwa na mshtuko na huzuni nyingi, nimejifunza kuhusu kufariki kwa Cyrus Jirongo ambaye alikuwa mtu muhimu kwa jamii yetu na Kenya. Tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi,’’ alisema Atwoli katik amtandao wa X.
Wasifu mfupi
Cyrus Shakhalaga Jirongo alikuwa mwanasiasa na mfanyabiashara mashuhuri wa Kenya.
Alipata umaarufu wa kitaifa mwanzoni mwa miaka ya 1990 kama mwenyekiti wa Youth for KANU ’92 (YK92), kikundi chenye nguvu cha ushawishi kilichofanya kampeni za kuchaguliwa tena kwa Rais Daniel arap Moi wakati Kenya iliporejea kwenye siasa za vyama vingi.
Alihudumu kama Mbunge wa Jimbo la Lugari, kwanza kutoka 1997 hadi 2002 na tena kutoka 2007 hadi 2013.
Wakati wa kazi yake ya kisiasa, aliteuliwa pia katika Baraza la Mawaziri ikiwemo wizara ya Maendeleo ya Vijijini.
Zaidi ya siasa, alijishughulisha na biashara na alibaki kuwa mtu mashuhuri katika maisha ya umma ya Kenya kwa miongo mingi hadi kifo chake.















