Mahakama Kuu ya Tanzania masijala ndogo ya Kigoma, imewahukumu kunyongwa hadi kufa maafisa watatu wa Uhamiaji kwa kosa la mauaji.
Fredrick Kyomo, Joachim Trathizius na Mabruki Hatibu, wanadaiwa kusababisha kifo cha Enos Elias, mkazi wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, kwa kudhania sio raia wa Tanzania.
Hukumu hiyo imetolewa Desemba 15, 2025, na Jaji Augustine Rwizile, ambapo amesema kuwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo umethibitisha pasi na kuacha shaka kuwa maafisa hao watatu walimuua Enos, kwa kumtuhumu kuwa si raia wa Tanzania.
Siku moja baadaye, inadaiwa kuwa ndugu zake walifika ofisi za uhamiaji wakiwa na kitambulisho cha utambulisho wa taifa, yaani NIDA cha Enos pamoja na barua ya utambulisho kutoka ofisi ya serikali ya mtaa.
Hata hivyo waliambiwa kuwa ndugu yao alikua amechiliwa huru, licha ya kutomkuta nyumbani wala kupatikana kupitia simu yake, hadi Oktoba 29, 2023, ulipookotwa porini ukiwa na majeraha.
Ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo unaonesha kuwa maafisa hao walitumia nguvu kupita kiasi na kumsababishia Enos mateso mbalimbali.
Inadaiwa kuwa, walifanya hivyo wakimlazimisha akiri kuwa yeye si Mtanzania.



















