Bunge la Zambia limeidhinisha kwa kwa kishindo siku ya Jumatatu muswada ambao utabadilisha vipengele vya katiba vinavyohusiana na katiba.
Upinzani unadai utaimarisha nafasi ya Rais Hakainde Hichilema katika uchaguzi wa mwakani, lakini serikali imekataa madai hayo, na Rais Hichilema akieleza kuwa mabadiliko hayo yamependekezwa kwa nia njema kwa faida ya muda mrefu kwa watu wa Zambia.
Wanasiasa wa upinzani, asasi za kiraia na makundi ya makanisa yalipinga muswada huo wa 7, wakisema kuwa uliharakishwa bungeni na kutoa nafasi kubwa kwa Hichilema na chama chake cha UPND katika uchaguzi wa Agosti 2026.
Muswada huo umefanyia marekebisho vipengele 13 vya katiba kwenye taifa hilo la Kusini mwa Afrika lenye utajiri mkubwa wa madini ya shaba, miongoni mwao kuongeza viti vya ubunge kutoka 156 hadi 226; kutenga viti 35 kwa ajili ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu; na kuondoa ukomo wa mihula miwili kwa mameya.
'Maagano na watu wa Zambia'
"Haya ni maagano na watu wa Zambian kuendeleza usawa," Waziri wa Haki Princess Kasune alisema baada ya bunge kuidhinisha kwa kura 131-2 vote, kumaanisha muswada huo sasa unahitaji saini ya Hichilema ili uwe sheria.
Wabunge Francis Kapyanga kutoka chama cha upinzani cha Patriotic Front (PF) alisema hawezi "kuhalalisha haramu."
Uhasama wa kisiasa katika nchi hiyo yenye watu milioni 22 ulijitokeza kuhusu mazishi ya mtangulizi wake Hichilema, Edgar Lungu, ambaye alifariki dunia katika hospitali nchi jirani ya Afrika Kusini mwezi Juni.
Familia ya Lungu ilikataa kuurejesha mwili wake kwa mazishi kwa sababu Hichilema alitaka kusimamia mazishi hayo.
'Changamoto' ya umoja wa kitaifa
Wakieleza kuhusu kuidhinishwa kwa Muswada wa 7, msemaji wa familia ya Lungu na mgombea wa urais kupitia chama cha PF Makebi Zulu alisema kwenye mtandao wa kijamii , "Mapambano ya demokrasia na heshima kwa utawala wa sheria yanaanza leo."
Hichilema – ambaye atagombea muhula wa pili wa miaka mitano kikatiba – alikiri kuwa muswada huo umeleta "changamoto" kwa umoja wa kitaifa lakini akasema matokeo ya kura ya bunge lazima yaheshimiwe.














