| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Mafuriko makubwa yamesababisha vifo vya takriban watu 21 katika eneo la Safi, Morocco
Morocco inakumbwa na mvua kubwa na theluji katika Milima ya Atlas, kufuatia miaka saba ya ukame ambao ulidhuru baadhi ya hifadhi zake kuu.
Mafuriko makubwa yamesababisha vifo vya takriban watu 21 katika eneo la Safi, Morocco
Morocco inashuhudia mvua kubwa na theluji katika Milima ya Atlas, kufuatia miaka saba ya ukame. / / AA
tokea masaa 3

Takriban watu 21 wamefariki dunia kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa katika mkoa wa Safi, ulioko kilomita 330 kusini mwa Rabat, nchini Morocco, mamlaka ya nchi hiyo imesema.

Mafuriko hayo pia yamejeruhi watu 32 siku ya Jumapili, na wengi wao wamepata matibabu na kutoka hospitalini, mamlaka imesema katika taarifa.

Mvua kubwa ya muda wa saa moja imeweza kusababisha mafuriko na kuharibu nyumba na maduka katika mji mkongwe wa Safi, kusomba magari na kuharibu barabara nyingi za Safi na mazingira yake, huku juhudi za uokoaji zikiendelea, mamlaka hiyo iliongeza.

Morocco inashuhudia mvua kubwa na theluji katika Milima ya Atlas, kufuatia miaka saba ya ukame.

CHANZO:Reuters