Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, na Waziri Mkuu wa Uingereza, Starmer, wamesaini mkataba wa ushirikiano wa pande mbili kuhusu ndege za Eurofighter Typhoon.
“Tunachukulia hili kama ishara mpya ya uhusiano wa kimkakati kati ya washirika wetu wa karibu,” Erdogan alisema baada ya kusaini makubaliano hayo na Starmer katika Ikulu ya Ankara.
Rais wa Uturuki alisema anaamini mkataba wa Eurofighter na Uingereza yatafungua mlango kwa miradi ya pamoja ya ulinzi. Erdogan pia alisema Uturuki na Uingereza zitaongeza kiwango cha biashara kifikie dola bilioni 40 na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi.
Starmer alisema mkataba huo una thamani ya karibu dola bilioni 11 za Marekani.
“Huu ni mkataba muhimu sana, kwa sababu ni mauzo yenye thamani ya dola bilioni 10.7; utatengeneza ajira ambazo zitaendelea kwa miaka 10,” alisema jijini Ankara, Uturuki.
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema kuwa mkataba huo ni ya ndege 20 za Eurofighter.
Siyo ndege tu
Wiki iliyopita, Mkurugenzi Mtendaji wa Ulinzi wa Airbus na Anga, Michael Schoellhorn alisema mkataba wa Eurofighter unaweza kuanzisha ushirikiano wa muda mrefu na Uturuki huku wakiendeleza aina mpya yenye kiwango cha juu zaidi kutumia teknolojia mpya.
Uturuki, ambayo ina jeshi la pili kubwa zaidi ndani ya muungano wa NATO, inapanga kununua ndege za kivita za Eurofighter Typhoon, ndege za kivita zenye uwezo tofauti zinazozalishwa kwa pamoja na Uingereza, Ujerumani, Italia, na Hispania.
“Eurofighter siyo ndege tu. Kuna mfumo ulioko nyuma yake. Kuna seti ya silaha iliyo nyuma yake. Katika siku za usoni, kutakuwa na muunganisho unaokuja nayo. Kutakuwa na suluhisho la ushirikiano kati ya binadamu na ndege zisizo na rubani,” Schoellhorn alisema, akimaanisha teknolojia mpya inayowezesha ushirikiano kati ya rubani na mfumi wa isiyoendeshwa na rubani zinazosimamiwa na hakili mnemba au mfumo wa kiotomatiki.
Ndege za Eurofighter Typhoon kwa sasa zinatumika na nchi tano za Ulaya: Uingereza, Ujerumani, Italia, Hispania, na Austria, pamoja na mataifa manne ya Ghuba, ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, Oman, Kuwait, na Qatar.

















