| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Watalii wawili wa Uturuki wauawa katika shambulio la risasi Ethiopia
Shambulio la risasi lilitokea katika eneo la vijijini karibu na mji wa Tum, Kusini-Magharibi mwa Ethiopia, huku uchunguzi bado unaendelea, kulingana na balozi wa Uturuki nchini Ethiopia.
Watalii wawili wa Uturuki wauawa katika shambulio la risasi Ethiopia
Miili ya wahasiriwa ilisafirishwa hadi Addis Ababa baada ya shambulio hilo. / / Reuters
14 Januari 2026

Raia wawili wa Uturuki pamoja na dereva ambaye ni raia wa Ethiopia wameuawa na majambazi wenye silaha walipokuwa katika safari ya utalii nchini Ethiopia, amesema balozi wa Uturuki jijini Addis Ababa.

Balozi Berk Baran aliiambia Shirika la Habari la Anadolu kwamba shambulio hilo la risasi lilitokea asubuhi ya Januari 12 katika eneo la vijijini karibu na mji wa Tum, kusini-magharibi mwa Ethiopia.

Waathirika waliyotambuliwa kuwa ni raia wa Uturuki ni Erdogan Akbulak na Cengizhan Gungor, pamoja na dereva wao ambaye ni raia wa Ethiopia, alisema Baran.

Kwa mujibu wa balozi, raia wanne wa Uturuki walikuwa wakisafiri kwa magari mawili tofauti wakati wa shambulio hilo. Watu wawili waliokuwa kwenye gari lililokuwa mbele waliweza kutoroka bila kujeruhiwa na baadaye wakatoa taarifa kwa ubalozi kuhusu tukio hilo.

Baran alisema kuwa raia wa Uturuki walionusurika pamoja na miili ya waliouawa ilisafirishwa kwa ndege hadi Addis Ababa asubuhi ya Jumanne.

“Taratibu zinaendelea. Raia wetu wanahifadhiwa katika ubalozi, na miili itasafirishwa kwenda Istanbul kwa ndege ya Turkish Airlines leo usiku, ikitarajiwa kuwasili kesho asubuhi,” Balozi huyo alisema.

CHANZO:AA
Soma zaidi
Rais wa Uturuki awasili Ethiopia kwa ziara rasmi
Emine Erdogan awatuza wasukuma mabadiliko wakati wa makala ya 7 ya tuzo za TRT World
Rais wa Uturuki aelekea Ethiopia kwa ziara ya kikazi
Waziri Mkuu wa Somalia apongeza uchimbaji mafuta wa 'kihistoria' baharini na Uturuki
Uturuki inapanua utaalam wa reli, kutoa mafunzo kwa wafanyakazi Afrika, Asia
Erdogan: Uturuki inaendelea kutafuta amani ya kanda licha hofu iliyopo ulimwenguni
Rais wa Uturuki ateuwa Waziri mpya wa Katiba na Mambo ya Ndani katika mabadiliko ya Baraza la Mawazi
Fidan wa Uturuki akataa mashambulizi ya anga kama njia ya kubadilisha uongozi wa Iran
Makamu wa Rais wa Uturuki akutana na balozi wa Brazil
Idadi ya watu nchini Uturuki yafikia milioni 86 kwa mwaka 2025
Uturuki yalaani shambulizi la RSF nchini Sudan
Matetemeko ya ardhi ya Uturuki 2023 yalisababisha hasara ya dola bilioni 250: Erdogan
Fidan wa Uturuki akutana na Kamishna wa Maswala ya Wanachama wa EU, kujadili masuala ya ushirikiano
Rais wa Uturuki aadhimisha kumbukumbu ya miaka 3 ya tetemeko la ardhi
Uturuki imelaani shambulizi la kigaidi nchini Nigeria lililoua takriban watu 170
Uturuki kuimarisha uwepo wake wa kijeshi kuisaidia Somalia kupambana na ugaidi
Uturuki na Saudi Arabia kuimarisha ushirikiano wa ulinzi na uwekezaji katika ndege za kivita za KAAN
Mke wa Rais wa Uturuki amekutana na mwenzake wa Misri jijini Cairo
Erdogan na Sisi waimarisha ushirikiano kati ya Uturuki na Misri wajadili Gaza na migogoro ya kikanda
Kikao cha mwisho cha Jukwaa la Biashara kati ya Uturuki na Misri chafunguliwa jijini Cairo