Marekani “imepongeza” makubaliano ya kusitishwa mapigano kwa muda yaliyofikiwa mapema siku ya Ijumaa Aleppo kufuatia kujiondoa kwa kundi la kigaidi la YPG.
Tom Barrack, mjumbe wa Marekani kuhusu Syria, alisema katika mtandao wa kijamii wa X kuwa Marekani “imepongeza makubaliano ya kusitishwa mapigano yaliyofikiwa jana usiku” katika maeneo ya Ashrafiyeh na Sheikh Maqsoud, akiyaeleza kuwa ni hatua muhimu iliyofikiwa kutokana na ushirikiano miongoni mwa pande zinazozozana.
YPG ni tawi la Syria la kundi la kigaidi la PKK.
Barrack alisema kuwa kusitishwa mapigano ilikuwa matokeo ya ‘‘kujizuia na utashi” na kueleza matumaini kuwa ushirikiano utafanya kuwepo kwa utulivu zaidi.
Alieleza makubaliano hayo kama hatua muhimu katika kuelekea kupatikana utulivu, akisema yanalenga kutoa muelekeo kwa jamii mbalimbali za Syria “kuwa na mtazamo mmoja wa upatikanaji wa usalama, ujumuishaji, na amani ya kudumu,” huku akikiri kuwa bado kuna changamoto.
Barrack amesema Marekani inajitahidi kuona kuwa usitishwaji wa mapigano unakwenda zaidi ya saa tatu asubuhi (0500 GMT) na kuendeleza kile alichokieleza “kuwa ari ya makubaliano.”
Mapigano zaidi
Jeshi la Syria limeshambulia kwa mabomu maeneo ya YPG Aleppo katika hatua ya kulipiza kisasi kutokana na mshambulizi yaliyowaua raia tisa na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Machi 10 2025, ofisi ya rais wa Syria ilitangaza kutiwa saini kwa makubaliano ya kundi hilo kujumuishwa kwenye taasisi za serikali, ikisisitiza kuhusu umoja wa maeneo ya nchi hiyo na kukataa majaribio yoyote ya mgawanyiko.
Mamlaka zinasema katika kipindi cha miezi kadhaa, kundi la kigaidi la YPG halijaonesha juhudi zozote za kutekeleza makubaliano hayo.
Serikali imezidisha juhudi za kuhakikisha kuna usalama nchini kote tangu kuondolewa kwa utawala wa Bashar al Assad Disemba 8 2024, baada ya miaka 24 madarakani.




















