MICHEZO
1 dk kusoma
Liverpool ina matatizo gani na Arne Slot anaweza kutatua mambo?
Wasiwasi umejiri kuhusu meneja wa Liverpool Arne Slot baada ya kufungwa nyumbani na Manchester United, ikiwa wapoteza mechi ya nne mfululizo katika mashindano yote.
Liverpool ina matatizo gani na Arne Slot anaweza kutatua mambo?
Meneja wa Liverpool Arne Slot. / Reuters
20 Oktoba 2025

Liverpool imepoteza michezo yake minne kwa tofauti ya goli moja tu na huenda wangeshinda mechi zote iwapo wangekuwa na jitihada zaidi katika umalizaji.

Lakini kuna kitu hakiko sawa kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England msimu huu.

Kwa hiyo Liverpool ina tatizo gani? Slot anaweza kutatua tatizo hilo haraka? Je wataendelea kuhangaika?

Ni wazi kuwa msimu huu Liverpool haijaweza kuwa na uwezo wa kuridhisha na mara nyingi wanakabiliwa vilivyo.

Wakati wa meneja Jurgen Klopp, Liverpool ilijulikana kwa kupambana kuanzia mwanzo, hili liliwasaidia kupata magoli mapema na kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza walikuwa wameshamaliza kazi. Sasa hivi hilo ni kama kitu kigeni kwao.

Wakati wa mechi yao na Manchester United, washambuliaji wanapotafuta magoli mbele, wachezaji wa nafasi ya kiungo walikuwa wanakaba katikati, wengine hawakufuata timu mbele kuongeza shinikizo. Kulikuwa na nafasi nyingi za wazi.

Wachezaji hawakuwa wanaelewana. United wakawa wanawachachafya katika maeneo yao. Inaonekana rahisi kupenya kwenye safu ya ulinzi ya Liverpool kama ilivyokuwa kwenye mechi zao dhidi ya Bournemouth, Crystal Palace na Chelsea kwa namna ilivyowapa tabu vijana wa Slot.

Ili kurejea katika hali yao ya kawaida, Liverpool inatakiwa kuhakikisha mpira unakuwa kwenye maeneo ya wapinzani wao zaidi na kuhakikisha hakuna hatari katika lango lao.

CHANZO:TRT Afrika Swahili