Wanaozika wagonjwa wa Ebola DRC wakabiliwa na unyanyapaa
AFRIKA
3 dk kusoma
Wanaozika wagonjwa wa Ebola DRC wakabiliwa na unyanyapaaIli kutokomeza maambukizi, mpango wa Mazishi ya Heshima na Salama (DSB) umeunda timu zinazoshughulikia vifo katika maeneo ambayo timu rasmi za DSB hazipo.
Wanwake pia wako katika timu zilizoundwa rasmi za kuwazika waliokufa kwa eboal nchini DRC / Reuters (Wire)
 

Kikundi cha watu wanaoratibu mazishi kwa wagonjwa wa Ebola kwa kufuata taratibu zote salama na za heshima, kinajiandaa kuchukua maiti Novemba 17 huko Kokola, karibu na Beni, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Miongoni mwa wanakikundi hao yupo mwanamke anayeitwa Chimene Mwanaki, ambaye anapambana dhidi ya chuki na dhana potofu zinazoelekezwa kwa wanawake katika vita dhidi ya Ebola.

"Baadhi ya watu wanatuambia kuwa tunaweza hata kuua waume zetu (kupitia maambukizi) au kwamba hatutapata mtu yeyote wa kutuoa, kwa sababu wanafikiri sisi ndio tunaosambaza Ebola—ingawa sivyo ilivyo," anasema Mwanaki.

Maambukizi yanaendelea miezi sita baadaye

Miezi sita tangu mlipuko wa Ebola utangazwe nchini DRC, ugonjwa huo bado haujadhibitiwa huku juhudi za kuuzuia zikionekana kusuasua

Kulingana na takwimu za serikali, zaidi ya maambukizi 11,000 yameripotiwa, na karibu nusu ya walioambukizwa wamefariki dunia.

Huu ndio mlipuko mbaya zaidi kati ya milipuko 17 ya Ebola iliyowahi kutokea DRC na unaelekea kuzidi idadi ya vifo vilivyotokea katika mlipuko uliokumba Afrika Magharibi, ambao uliua watu 11,000 kati ya mwaka 2014 na 2016.

Ili kukata maambukizi, mpango wa Mazishi ya Heshima na Salama (DSB) umeunda timu zinazoshughulikia vifo katika maeneo ambayo timu rasmi za DSB hazipo.

Timu hizi za ndani zinaitwa 'Ecumair', yaani Timu za Kijamii kwa ajili ya Mazishi ya Heshima na Salama.

Wakati mlipuko huo ulipotangazwa katikati ya mwezi Mei, tayari watu 43 waliripotiwa kufariki kwa Ebola; jambo linaloashiria kuwa virusi hivyo vilikuwa vimeenea bila kugundulika kwa muda mrefu.

Maeneo mapya DRC yanaathiriwa

Tangu wakati huo, ugonjwa umeenea katika mikoa minane kati ya mikoa 26 ya nchi hiyo, ukienea kwa kasi.

Maeneo mapya yenye maambukizi yanaendelea kujitokeza, jambo linalozidi kulemea mfumo wa huduma za afya ambao tayari umeshinikizwa mno.

Jean Manina, msimamizi wa DSB katika eneo la afya la Oicha, alitembelea timu ya eneo hilo huko Erengueti ili kufuatilia na kuhakikisha kuwa kazi inafanywa kwa kuzingatia itifaki za mazishi.

Hii ni kwa ajili ya kuzuia wanachama wa timu hizo kuambukizwa wenyewe wakati wanapovua vifaa vyao vya kujikinga.

"Kila siku, jambo la kwanza ninalofanya ni kuangalia mfumo wa ufuatiliaji wa taarifa. Ikiwa tunapata taarifa kutoka eneo la afya ambapo tuna timu ya ECUMAIR (Timu za Jamii kwa ajili ya Mazishi Salama na ya Heshima), lazima niende huko ili kuona jinsi wanavyotekeleza majukumu yao,” alielezea.

Kashfa ya watoa huduma

“Sasa, katika maeneo ambayo hatuna timu za ECUMAIR—yaani, sehemu nyingine za eneo la afya la Oicha—timu ya dharura inayohamishika iliyopo hapa ndiyo hutumwa," alisema Jean Manina, ambae ni msimamizi wa DSB katika eneo la afya la Oicha.

Mbali na hatari za kiafya na ukosefu wa muda wa kuwa na familia zao, timu hizi za mazishi wakati mwingine hushambuliwa na wanajamii wanaowatuhumu kuharibu miili ya waliokufa.

Hii inatokana na ukweli kwamba wanachukua sampuli ili kupima kama Ebola ndiyo iliyosababisha kifo.

Lakini mara nyingi, wanachama wa timu hizi hukabiliwa na chuki hata ndani ya mitaa wanayoishi.

"Tunapokuwa nyumbani, majirani zetu hutuambia: 'Ninyi ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na ugonjwa huu, kwa hivyo mnapata pesa. Mnawezesha wazungu kuua raia wenzetu. Hata hivyo, hilo si kweli—tunapambana ili kutokomeza maambukizi ya Ebola," alisema Jean Manina.

CHANZO:AP (Wire)