Waziri wa Mambo ya Nje wa Eritrea Osman Saleh amekutana na mwenzake wa Misri Badr Abdelatty jijini Cairo siku ya Jumatano kujadili masuala yanayohusu mataifa yao mawili na yanayojiri katika kanda, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ilisema.
Viongozi hao walijadili vita vinavyoendela nchini Sudan, oparesheni za kukabiliana na ugaidi Somalia, usalama katika Bahari ya Shamu na kuimarisha ushirikiano kati ya Misri, Eritrea na Somalia.
Mkutano huu unajiri baada ya Eritrea na Ethiopia kusitisha uhusiano wa kidiplomasia mapema mwezi Oktoba 2026 kufuatia uamuzi wa Ethiopia kufunga ubalozi wake mjini Asmara na kuwafukuza wanadiplomasia 10 wa Eritrea, wakidai kuwa “ni tishio” kwa usalama wa taifa lao.
Eritrea inakanusha kuingilia masuala ya ndani ya Ethiopia.











