| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Saadaq Omar ateuliwa waziri wa ulinzi katika mabadiliko ya baraza nchini Somalia
Uteuzi huo unakuja huku Somalia ikijiandaa kwa hatua muhimu katika mipango yake ya kiusalama.
Saadaq Omar ateuliwa waziri wa ulinzi katika mabadiliko ya baraza nchini Somalia
Mabadiliko ya uongozi yanakuja huku Somalia ikiimarisha uwezo wa majeshi yake. / Bunge la Somalia
 

Waziri Mkuu wa Somalia Hamza Abdi Barre siku ya Jumatatu amemteua Saadaq Omar Mohamed Hassan, maarufu Saadaq Joon, kuwa waziri wa ulinzi mpya wa nchi hiyo, akichukua nafasi ya Ahmed Moallim Fiqi katika mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri wakati serikali ikiimarisha vikosi vyake vya usalama kwenye oparesheni dhidi ya magaidi wa Al-Shabaab.

Uteuzi huo, uliotangazwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, unakuja huku Somalia ikijiandaa kwa hatua nyingine ya kuimarisha usalama, ikiwemo majadiliano kuhusu mustakabali wa vikosi vya Umoja wa Afrika (AUSSOM).

Saadaq, ambaye ni mbunge wa bunge la Somalia, anamrithi Fiqi, alieongoza Wizara ya Ulinzi tangu tarehe 27 Aprili 2025.

Mabadiliko hayo pia yanajumuisha nafasi mbili za manaibu waziri.

Ali Ifiye Ali ameteuliwa kuwa naibu waziri wa bandari na usafiri wa baharini, huku Maryan Ali Abukar akipewa majukumu ya unaibu waziri wa uvuvi.

Ofisi ya Waziri Mkuu imeagiza walioteuliwa kuanza majukumu yao mara moja na kufanya kazi kwa weledi, uwazi na uwajibikaji.

CHANZO:TRT Afrika Swahili