Rais wa Burkina Faso Ibrahim Traoré amezindua mradi mwingine wakati nchi hiyo ya Afrika Magharibi inapojiimarisha na agenda yake ya kujitegemea.
Chuo cha Teknolojia cha Burkina Faso kilijengwa katika kipindi cha chini ya miezi 11.
Wakati wa ufunguzi mjini Ouagadougou tarehe 23 Novemba, Traoré alisema kuwa mradi huo "unasisitiza dhamira ya Burkina Faso na ari ya kukumbatia sayansi kwa ajili ya mustakabali wake."
Chuo hicho kinatarajiwa kujihusisha na vifaa vya teknolojia katika viwanda, ikiwemo elektroniki.
Kiongozi huyo wa Burkina Faso pia aliwataka wanafunzi kujitahidi "kufaulu zaidi", na kutokuwa na mipaka katika ubunifu wao, pamoja na kuzingatia kauli mbiu ya kituo hicho ya: Werevu – Ujasiri – Nidhamu.
‘Hakuna tena mafunzo ya nje’
Hili, kulingana na yeye, ni muhimu kwa sababu "watu ambao hawana ujasiri hawawezi kuimarisha sayansi au kuwa na maendeleo."
Chuo hicho kinalenga kuwapa mafunzo wahandisi wa ngazi za juu na watafiti kuhusu “vipaumbele vya taifa” — kuanzia teknolojia ya kidijitali na utengenezaji wa ndege, nishati hadi kilimo, uchimbaji madini, sayansi ya kompytuta na ya nyuklia, serikali imesema.













