8 Januari 2026
Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan siku ya Alhamisi alimpokea Philippe Lazzarini, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi wa Palestina (UNRWA), katika sehemu ya wageni ya ikulu ya rais jijini Ankara.
“Nimefurahi kukutana na Philippe Lazzarini, Kamishna Mkuu wa (UNRWA). Natumai kuwa ile kazi inayofanywa kwa dhati kwa ajili ya watu wa Palestina itakuwa na tija na matokeo mazuri ya kudumu ambayo yatamaliza madhila yao,',” Erdogan aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Uturuki NSosyal.
ZILIZOPENDEKEZWA
Lazzarini, naye, alieleza shukrani zake, akieleza kuhusu uongozi wa mke wa Rais katika suala la Palestina.
Balozi Mehmet Gulluoglu, mratibu wa Uturuki kwa masuala ya misaada ya watu wa Palestina, pia alikuwepo kwenye mkutano huo.
CHANZO:AA




















