| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
8 wapoteza maisha katika ajali ya helikopta nchini Peru
Chanzo cha ajali hiyo, bado hakijajulikana, kwa mujibu wa mamlaka za nchi hiyo.
8 wapoteza maisha katika ajali ya helikopta nchini Peru
Chanzo cha ajali hiyo, bado hakijajulikana, kwa mujibu wa mamlaka za nchi hiyo. / Others
 

Watu nane wamepoteza maisha baada ya helikopta ya kijeshi ya Peru kudondoka kwenye bonde la Mantaro, siku ya Ijumaa.

Kulingana na Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo, vikosi vya uokoaji vilifanikiwa kupata mabaki ya helikopta hiyo, huku rubani wake akiwa ni mtu pekee aliyepona katika ajali hiyo.

Chanzo cha ajali hiyo, bado hakijajulikana, kwa mujibu wa mamlaka za nchi hiyo.

Kupitia taarifa yake iliyotolewa siku ya Ijumaa, Kamandi Maalumu ya VRAEM, ilisema kuwa, ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Sanabamba, katika mkoa wa Ayacucho uliopo kusini mwa Peru.

Eneo hilo, linajulikana zaidi kwa uzalishaji wa kokeini.

CHANZO:Anadolu Agency