| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki yapanua mtandao wa reli kwa asilimia 30 katika miaka 25
Treni za mwendo kasi za moja kwa moja sasa zinahudumia majimbo 14, na wizara ya uchukuzi inapanga kupanua huduma hizo hadi majimbo 18 zaidi kufikia mwaka 2030.
Uturuki yapanua mtandao wa reli kwa asilimia 30 katika miaka 25
Abiria wakipanda treni kwenye njia ya Cerkezkoy–Kapikule kaskazini-magharibi mwa Uturuki. Picha/Maktaba / AA Archive
 

Uturuki imepanua mtandao wake wa reli kwa takriban asilimia 30 tangu mwaka 2002 na kuboresha miundombinu yake ya reli, Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu, Abdulkadir Uraloglu, ameliambia shirika la habari la Anadolu.

Uraloglu amesema mtandao huo umekua kutoka kilomita 10,948 mwaka 2002 hadi kilomita 14,272 mwaka huu.

Kwa sasa mtandao huo una kilomita 11,668 za reli za kawaida na kilomita 2,604 za reli za mwendokasi, ambapo za mwendokasi zote zimejengwa tangu mwaka 2002.

Reli zinazotumia umeme zaongezeka zaidi ya mara tatu

Urefu wa njia za reli zinazotumia umeme umeongezeka kwa asilimia 259, kutoka kilomita 2,122 hadi kilomita 7,627. Mitandao ya reli za mijini imekua kwa asilimia 276, kutoka kilomita 281 hadi kilomita 1,056, amesema Uraloglu.

"Kazi ya usanifu wa miradi imekamilika kwenye kilomita 8,458, na juhudi zinaendelea kwenye njia yenye urefu wa kilomita 3,985."

"Jumla ya urefu wa reli itafikia takriban kilomita 31,439 pindi miradi yote iliyopangwa itakapokamilika," amesema.

Huduma za treni za mwendokasi zapangwa kufika mikoa 18 zaidi

Treni za moja kwa moja za mwendokasi zinahudumia mikoa 14, na Wizara inapanga kufikisha jumla ya mikoa 32 ifikapo mwaka 2030, amesema Uraloglu.

"Tunatoa huduma ya moja kwa moja ya reli ya mwendokasi katika mikoa ya Istanbul, Kocaeli, Eskisehir, Yozgat, Kirklareli, Ankara, Konya, Karaman, Sivas, Tekirdag, Sakarya, Bilecik, Kirikkale na Edirne.

"Tutaongeza Bursa, Corum, Kayseri, Nigde, Izmir, Usak, Balikesir, Afyonkarahisar, Mersin, Adana, Osmaniye, Gaziantep, Adiyaman, Manisa, Malatya, Kahramanmaras, Igdir na Kars kwenye orodha hiyo ifikapo mwaka 2030," ameongeza.

Chanzo: Anadolu