| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Hati ya kukamatwa kwa mtoto wa Robert Mugabe yatolewa baada ya kukosa kufika mahakamani
Bellarmine Chatunga Mugabe alikosa kufika mahakamani katika kesi inayohusisha wizia wa mabavu na kuharibu mali.
Hati ya kukamatwa kwa mtoto wa Robert Mugabe yatolewa baada ya kukosa kufika mahakamani
PICHA YA MAKTABA: Bellarmine Chatunga Mugabe ana historia ya ukiukaji wa sheria. / Reuters (Wire) / Reuters (Wire)
 

Mahakama nchini Zimbabwe imetoa hati ya kukamatwa kwa mtoto wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe baada ya kutohudhuria kikao cha kesi inayomhusu siku ya Jumanne.

Bellarmine Chatunga Mugabe, mtoto wa kiume wa Mugabe, alikamatwa mapema mwezi huu pamoja na watu wengine wanne kwa madai ya kumshambulia askari polisi.

Kukamatwa huko ilikuwa kwa uchunguzi kuhusu madai ya biashara ya magendo ya magari ya kifahari.

Watano hao wanakabiliwa na mashtaka ya wizi wa mabavu na kuharibu mali na walipewa dhamana tarehe 6 Novemba, huku wakitakiwa kufika mahakamani siku ya Jumanne.

Hata hivyo, Mugabe hakufika kwa kikao hicho, huku washtakiwa wenzake, msaidizi wake na walinzi watatu, wakifika na kupelekwa rumane hadi Disemba 10.

Matatizo na sheria

Bellarmine Chatunga amekuwa akimulikwa katika miaka ya hivi karibuni kutokana na ukiukaji wa sheria na maisha yake binafsi, ikiwemo kukiri matumizi ya bangi.

Mwezi Aprili mwaka huu, alitimuliwa kutoka nchi jirani ya Afrika Kusini baada ya kukiri kumtishia mtu silaha na kuwa nchini kinyume cha sheria.

Alikuwa amekamatwa kufuatia tukio la kumfyatulia risasi mtu mmoja mwenye umri wa miaka 23 nyumbani kwake.

Mwaka 2023, alikamatwa katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, kwa madai ya kuharibu mali na kumtemea mate polisi wakati wa sherehe.

 

CHANZO:َAA