| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Waombolezaji watatizika kupata miili ya jamaa zao waliofariki kwa Ebola
Watu wamekusanyika nje ya mochwari ya hospitali kubwa mji wa Beni, wakishtumu kile walichosema ni namna maiti za watu zinavyohifadhiwa.
Waombolezaji watatizika kupata miili ya jamaa zao waliofariki kwa Ebola
PICHA YA MAKTABA: Wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu wakibeba jeneza la mtu aliyefariki kwa virusi vya Ebola kabla ya kumzika. / Reuters (Wire / Reuters (Wire)
 

Wakazi kadhaa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema wamekuwa wakitatizika kubaini ilipo miili ya jamaa zao waliofariki kutokana na mlipuko wa Ebola, huku wengine wakisema wapendwa wao wamezikwa bila wao kupewa taarifa.

Watu wamekusanyika nje ya mochwari ya hospitali kubwa mji wa Beni, mkoa wa Kivu Kaskazini wakishtumu kile walichosema ni namna maiti za watu zinavyohifadhiwa.

Wahudumu wa afya, wanaozika na mamlaka za serikali za mitaa waliziambia familia kuwa wanajitahidi kubaini sehemu miili ilipo.

Matukio hayo yamesababisha watu kutokuwa na imani na vituo vya afya katika eneo hilo ambalo wahudumu wanaoshughulikia tatizo la Ebola wamekuwa hawaaminiwi na wakati mwingine kushambuliwa na watu.

Mji wa Beni umekuwa na maambukizi zaidi ya Ebola kuliko eneo lolote tangu mwanzo wa mwezi Novemba, ikiwa ni karibu na humusi ya maambukizi yote yaliyorekodiwa katika kipindi hicho, kulingana na takwimu za serikali.

CHANZO:TRT Afrika Swahili