UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki na Jordan zasaini makubaliano ya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi
Mkutano huo umeashiria hatua muhimu katika uhusiano wa mataifa hayo mawili, ukijumuisha ushirikiano katika biashara, uwekezaji, miundombinu, kilimo, afya, na utamaduni.
Uturuki na Jordan zasaini makubaliano ya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi
Kiwango cha biashara cha Uturuki na Jordan kilifikia karibu dola bilioni 1.5 kati ya Januari na Septemba. / / AA
tokea masaa 8

Uturuki na Jordan zimesaini makubaliano ya ushirikiano katika mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kiuchumi ya Uturuki–Jordan (JEC) uliofanyika mjini Amman, Jordan, kwa ushiriki wa mawaziri wa biashara wa nchi hizo mbili.

Waziri wa Biashara wa Uturuki, Omer Bolat, alisema katika hafla hiyo kwamba mkutano wa JEC ni hatua ya kihistoria katika uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, hasa katika nyanja za biashara, uwekezaji, miundombinu, ujenzi, kilimo, afya, utamaduni, utalii na nyanja zingine, kufuatia kusainiwa kwa tume ya kwanza ya pamoja ya kiuchumi.

Bolat alibainisha kuwa katika mikutano ya mataifa mawili, pande zote mbili — Uturuki na Jordan — zimekubaliana kuanzisha miradi na programu mpya za ushirikiano katika maeneo muhimu.

Wafanyabiashara wa Kituruki na wa Kijordan, pamoja na Bodi ya Mahusiano ya Kiuchumi ya Nje (DEIK), walifanya kikao cha majadiliano kama sehemu ya ziara ya Bolat, huku jumuiya za biashara za nchi hizo zikitarajiwa kukutana tena katika kongamano maalum siku za usoni.

Bolat alisema, “Tutatia saini makubaliano mengi ya ushirikiano katika sekta ya biashara huria, biashara ndogo, maeneo ya viwanda vilivyo tayarishwa, viwango vya ubora, elimu, afya na utafiti wa kisayansi, pamoja na kilimo.”

Kiasi cha biashara kati ya Uturuki na Jordan kilifikia takriban dola bilioni 1.5 kati ya Januari na Septemba, ishara ya ukuaji wa haraka wa uhusiano wa kibiashara unaoongozwa na kufaidisha pande zote, aliongeza Bolat.

Alisisitiza kuwa Uturuki na Jordan, pamoja na sekta binafsi za nchi hizo, zinaunga mkono ushirikiano katika juhudi za ujenzi upya wa Syria, Ukanda wa Gaza wa Palestina, na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.

Bolat alihitimisha kwa kusema kuwa njia ya usafiri ya kihistoria kati ya Syria na Jordan itaimarisha usafirishaji na biashara kutoka Ulaya hadi Ghuba kupitia Uturuki, Syria, na Jordan, kisha kurudi tena Ulaya.

CHANZO:AA