Polisi katika Jimbo la Nigeria la Edo wameanzisha msako wa watu watatu waliowafytulia risasi wafuasi wa chama cha Nigeria Democratic Congress (NDC) mjini Benin, kusababisha mtu mmoja kujeruhiwa, huku mashambulizi ya kisiasa yakizua wasiwasi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Mashambulizi yote yalitokea siku ya Jumatano, tarehe 25 Novemba, wakati wa mkutano wa mgombea Urais Peter Obi, katika jimbo hilo.
Polisi wa Jimbo la Edo wanasema waliohusika waliwasili na gari aina nyeusi aina ya Toyota Hilux na kufyatua risasi baada ya kuona maafisa wa polisi katika mlango wa uwanja wa ndege.
“Waliwapowaona maafisa wa polisi katika mlango wa kutokea wa Uwanja wa Ndege, na kugundua hawawezi kupiga hatua, waligeuka na kuwafyatulia watu risasi kabla ya kukimbia,” polisi walisema katika taarifa kwenye mtandao wa X.
Mtu mmoja alijeruhiwa kwa risasi kwenye mapaja yake na kupelekwa hospitali, ambako anatibiwa.














