Hamisi Iddi Hamisi akiwa Morocco
Dakika 45 za mwanzo zilianza kwa papatu papatu za kila upande kutengeneza nafasi za kufunga lakini milango ilikuwa migumu.
Ikumbukwe kuwa Senegal iliwatupa nje Misri kwenye fainali ya AFCON 2021 kwa matuta 4-2 na kutwaa ubingwa huo. Timu zote zikiwa na nyota waliong’ara wakiwa Pamoja katika ligi ya England ya Liverpool, Mohamed Salah na Sadio Mane wa Senegal walikuwemo katika mchezo huo uliojaa hisia.
Bila shaka Mafarao walitaka kumaliza uteja na kulipiza kisasi kwa ‘Simba wa Teranga’, lakini pia akina Sadio Mane na Kalidou Koulibaly walitaka kuendeleza kichapo kwa Misri.
Kipindi cha awali kiliisha kwa timu zote kutoshana nguvu matokeo yakiwa 0-0.
Kipindi cha pili: Mbabe lazima aptikane
Ndipo dakika za 45 za kipindi cha pili zilianza kwa mashambulizi ya kasi timu zote zikijaribu mbinu za kupenya safu ya ulinzi.
Senegal ambao walionekana kumiliki mchezo sehemu ya kati wakipiga pasi maridhawa na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.
Mashabiki zaidi ya 50,000 walifika kutazama mtanange huu uliojaa hisia za kuhistoria na heshima.
Bao la lilipatikana dakika 78 ya mchezo, ambapo Sadio Mane aliipatia Senegal alipotandika mkwaju mkali nje ya eneo la kumi na nane na kutikisa wavu.
Huku Misri wakipambana kurusiha goli hili ili mchezo uendelee ilishindikana kwani Senegal walikuwa makini kuzuia.
Hadi Kipyenga cha mwamuzi kinapulizwa kuashiria kumalizika kwa dakika 90 za mchezo, mbabe alikuwa ni Senegal kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0.
Jumapili atakabiliana na wenyeji wa makala haya ya 35 Morocco.




















