Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ametangaza washindi wa Tuzo Kuu za Utamaduni na Sanaa za Urais za mwaka 2025 katika hafla maalum ya kuadhimisha Siku ya Jamhuri iliyofanyika katika Ikulu ya Rais jijini Ankara, Uturuki.
Erdogan amesema siku ya Jumatano kwamba tuzo katika kategoria ya “Sayansi na Utamaduni” imetolewa kwa msomi Suleyman Seyfi Ogun, huku Yalcin Gokcebag akitambuliwa katika kategoria ya “Uchoraji”, mtunzi wa muziki Yalcin Tura katika kategoria ya “Muziki”, na mwanaakiolojia na mhadhiri Fahri Isik katika kategoria yaa “Akiolojia ya Anatolia.”
Aidha, tuzo katika kategoria ya “Upigaji Picha” amepewa mpiga picha wa shirika la habari la Anadolu, Ali Jadallah, anayefanya kazi huko Gaza.
Rais Erdogan pia alitangaza kwamba Tuzo ya Kimataifa ya Amani ya Ataturk kwa mwaka huu itatolewa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.

















