| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Ndege mbili za Kimarekani zagongana mbawa zikiwa ardhini
Hata hivyo, tukio hilo, halikuathiri ratiba za ndege zingine, na huduma za usafiri ndani ya uwanja huo.
Ndege mbili za Kimarekani zagongana mbawa zikiwa ardhini
Hata hivyo, tukio hilo, halikuathiri ratiba za ndege zingine, na huduma za usafiri ndani ya uwanja huo. / Others
 

Ndege mbili zinazomilikiwa na Shirika la American Airlines, zimegongana mbawa, wakati zikiwa ardhini kwenye uwanja wa Ronald Reagan, siku ya Ijumaa.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Usalama wa Anga ya Marekani, tukio hilo lilihusisha ndege namba 638 na 2152, wakati zikijiandaa kwa miruko.

Hata hivyo, hakuna taarifa zozote za majeruhi, kulingana na mamlaka hiyo.

Katika taarifa yake kwa chombo cha habari cha CBS, American Airlines, ilithibitisha kutoka kwa ajali, kabla ya ndege hizo kurudishwa kwenye yadi maalumu kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hata hivyo, tukio hilo, halikuathiri ratiba za ndege zingine, na huduma za usafiri ndani ya uwanja huo.

Wakati ndege namba 638 ilikuwa na ratiba ya kuelekea kwenye jiji la Dallas, ile ya 2152 ilipangwa kusafiri hadi Chicago.

CHANZO:Anadolu Agency