Misaada yapungua Sudan Kusini huku waliopoteza makazi wakikabiliana na majanga
AFRIKA
2 dk kusoma
Misaada yapungua Sudan Kusini huku waliopoteza makazi wakikabiliana na majangaWamejikuta katikati ya mzozo na athari za tabianchi, jamii za waliopoteza makazi yao Sudan Kusini zinajikuta zikikabiliana na vurugu, mafuriko na kukosa misaada ya kutosha
Kufurika kwa mito katika wiki za hivi karibuni, kumesababisha watu zaidi 100,000 kuondoka katika makazi yao. Picha: UNHCR/Tiksa Negeri / Wengine
tokea masaa 12

Adhieu Marial amesimama kwa kile kilichobaki kwa nyumba yake katika Jimbo la Unity la Sudan Kusini, akitathmini kilichobaki baada ya mafuriko.

"Kwanza, tumekimbia mashambulizi ya risasi. Sasa,tunakimbia maji," mama huyo mwenye watoto wanne ameiambia TRT Afrika.

Katika wiki za hivi karibuni, mito iliyofurika imefunika sehemu kubwa ya majimbo ya Jonglei, Upper Nile na Unity, na kusababisha watu zaidi ya 100,000 kuachwa bila makazi yao. Wengi wao walikuwa ndiyo wanaanza tu kujenga upya maisha yao baada ya kulazimika kukimbia mapigano yaliyotibuka mapema mwaka huu.

Sasa, mafuriko yana watatiza tena.

Adhieu, ni miongoni mwa wale wanaojaribu kuweka sawa maisha yao huku wakikabiliana na janga lingine, ameamua kuangazia mustakabali wake.

"Mafuriko yalifunika nyumba yetu, lakini bado tuna matumaini. Kwa mabati haya tuliyopata kutoka kwa mashirika ya misaada, angalau tumepata sehemu ya kujistiri. Watoto wangu wako salama kwa sasa," anasema Adhieu, akiwa anawakilisha hisia za maelfu ya watu.

Matatizo mbalimbali

Kila siku, kuna matumaini kwa wale waliopoteza makazi yao Sudan Kusini.

Shirika linaloshughulikia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limeonya kuwa kama mafuriko yataendelea, watu hadi ya 400,000 watakuwa wamepoteza makazi yao kufikia mwisho wa mwaka.

"Tunakabiliwa na matatizo ya mabadiliko ya tabianchi na migogoro, ambapo tatizo moja linasababisha tatizo lingine," Eunice Njeri, mratibu anayefanya kazi na mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya kiserikalli Sudan Kusini, ameiambia TRT Afrika.

"Familia moja iliyopoteza makazi yake kutokana na vita inafika katika eneo lingine, na wanapata mkosi wa kuondoka pia kwenye sehemu hiyo kutokana na mafuriko.Kuhamahama huku kunafanya iwe vigumu kusaidia familia na kufanya hali kuwa ngumu zaidi kwa watu."

Suluhu, Njeri anasema, iko katika kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na matatizo badala ya kuyaangalia kama matatizo tofauti. "Misaada kutoka kwa jamii ya kimataifa yanatakiwa kuwa mahsusi kwa ajili ya migogoro wanayopitia watu hawa," anasema.

Elimu

Huku kukiwa na changamoto, kuna matumaini katika suala la elimu.

Walimu wana matumaini ya kuendeleza elimu hata wakati shule na madarasa yakigeuka kuwa vidimbwi.

"Hii ni changamoto kubwa," anasema Puot Kuol, mwalimu huko Upper Nile. "Lakini hatuwezi kukata tamaa. Vita vimetatiza elimu, na sasa mafuriko yamesababisha changamoto nyingine. Lakini sasa tunatafuta suluhu – kufunza chini ya miti, ndani ya hema lilitolewa la msaada, popote tunapoweza. Watoto hawa ni mustakabali wa Sudan Kusini. Tutapata njia ya kuwafunza."

CHANZO:TRT Afrika