Balozi wa Uturuki nchini Syria Nuh Yilmaz alisema siku ya Ijumaa kuwa inaridhisha kuona kuwa makubaliano ya Aprili 1 hatimae yanatekelezwa Aleppo, Syria.
“Inaridhisha kuona kuwa makubaliano ya Aprili 1, ambayo yanalenga kupatikana kwa amani na utulivu Aleppo, hatimae yanatekelezwa, ingawa kwa kuchelewa na kwa uzito,” Yilmaz alisema katika ujumbe kupitia mtandao wa kijamii wa Marekani X.
Akieleza kuhusu makubaliano yaliyofikiwa mwaka uliopita kati ya serikali ya Syria na kundi la kigaidi la YPG/SDF kuhusu kundi hilo kuondoka maeneo ya Sheikh Maksoud na Ashrafiyeh Aleppo, Yilmaz alisema: “Usalama, umoja na utulivu utatupeleka katika kupatikana kwa mustakbali bora.”
Kundi la kigaidi la YPG/SDF limekuwa likishambulia maeneo kadhaa Aleppo kutoka maeneo ambayo wanayadhibiti tangu Disemba 6.
Jeshi la Syria lilishambulia maeneo ya YPG/SDF huko Aleppo wakilipiza kisasi cha mashambulizi yaliyowaua watu tisa na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Mwezi Machi mwaka uliopita, ofisi ya rais wa Syria ilitangaza kutiwa saini kwa makubaliano ya kujumuisha YPG/SDF kwenye taasisi za serikali, ikisisitiza kuhusu umoja wa nchi na kukataa majaribio ya kugawanywa.
Lakini miezi kadhaa tangu wakati huo, mamlaka zinasema, kundi hilo la kigaidi halijaonesha juhudi zozote za kutekeleza makubaliano hayo.
Serikali ya Syria imeendeleza juhudi za kupatikana kwa usalama kote nchini tangu kuondolewa kwa utawala wa Bashar al-Assad Disemba 8, 2024, baada ya kuwepo madarakani kwa miaka 24.




















