ULIMWENGU
2 dk kusoma
Kenya: Familia ya askari aliyepotea Haiti yashangwa baada ya kubaini kuwa alifariki dunia
Ruto alikiri kuwa afisa huyo aliaga dunia, jambo linalokinzana na matamshi ya awali ya maafisa wa serikali akiwemo Inspekta Jenerali ambaye alikanusha ripoti za kifo chake.
Kenya: Familia ya askari aliyepotea Haiti yashangwa baada ya kubaini kuwa alifariki dunia
Maafisa watatu wa Kenya wameuawa nchini Haiti/Picha Reuters
tokea masaa 7

Familia ya Benedict Kabiru, afisa wa polisi wa Kenya ambaye alikuwa ametoweka kwa muda wa miezi sita iliyopita tangu Machi 2025, imeshtushwa baada ya Rais William Ruto kuthibitisha kifo chake wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA).

Taarifa hii inajiri baada ya miezi kadhaa ya serikali kusisitiza kuwa Kabiru yuko hai na bado anafuatiliwa.

Rais Ruto alikiri kuwa afisa huyo aliaga dunia, jambo linalokinzana na matamshi ya awali ya maafisa wa serikali akiwemo Inspekta Jenerali ambaye alikanusha ripoti za kifo chake.

"Lazima nitumie tukio hii kuwaenzi maafisa wa Kenya Bw. Samuel Tuoi, Benedict Kabiru, na Kennedy Nzuve, ambao walipoteza maisha wakiwa kazini," Ruto alisema katika mkutano wa UN mjini New York.

Kabiru alitoweka baada ya maafisa wa polisi wa Kenya kuvamiwa na genge moja nchini Haiti.

Familia yake sasa inamtaka Rais Ruto kuratibu juhudi za kurudisha mwili wake nchini Kenya.

Nayo Huduma ya Polisi nchini imetoa taarifa sasa ya kutangaza kifo chake.

“Katika hali ya kusikitisha, Jeshi la Polisi la Taifa lilipokea taarifa kuhusu kifo cha afisa aliyetoweka,” imesema katika taarifa siku moja baada ya Rais Ruto kufichua kifo chake.

Jacinta Kabiru, ambae ni mama wa fisa huyo, aliikosoa serikali kwa kuwahadaa kwa miezi kadhaa.

“Sasa kwa nini wananitesa, kwanini wamenitesa muda wote huku wakijua vizuri, najua Rais hawezi kutoa taarifa zisizo za kweli, nawaomba, walete mabaki ya mwanangu ili nifanye kinachohitajika, maana siamini mpaka niuone,” alisema.

Kufikia sasa, maafisa watatu wa polisi wa Kenya wamepoteza maisha yao nchini Haiti walipokuwa wakihudumu chini ya ujumbe wa Multinational Security Support (MSS).

Wa kwanza alikuwa Samuel Tompei Kaetuai, aliyeuawa Februari 2025.

Benedict Kabiru naye inaripotiwa alivamiwa na magenge.

Mkasa wa hivi majuzi zaidi ulitokea Septemba 2025, wakati Koplo Kennedy Mutuku Nzuve alipofariki katika ajali ya gari la kivita.

Huduma ya Polisi nchini imesema mwili wake Nzuve utawasili nchini Kenya kutoka Haiti Septemba 26, 2025.

CHANZO:TRT Swahili