| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Uturuki yatuma salamu za rambirambi Misri kufuatia ajali ya lori la mafuta
Mamlaka za nchini Misri zinasema zimemkamata dereva wa gari anayeshukiwa kusababisha kupinduka kwa lori la mafuta katika barabara kubwa.
Uturuki yatuma salamu za rambirambi Misri kufuatia ajali ya lori la mafuta
Maafisa wa zimamoto walifanikiwa kuuzima moto na kuwatoa watu kwenye magari yaliyoungua. / Anadolu Agency (Wire) / Anadolu Agency (Wire)
 

Siku ya Alhamisi Uturuki ilitoa salamu zake za rambirambi kwa Misri kufuatia ajali ya lori la mafuta iliyowaua watu 31 na kuwajeruhi wengine.

Katika taarifa, Wizara ya Mambo ya Nje ilieleza huzuni wake kwa watu kupoteza maisha katika tukio hilo la Jumatano mkoa wa Giza.

“Tunamuomba Mungu awarehemu wale waliopoteza maisha yao katika ajali, tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa jamaa zao na watu wa Misri, na tunawaombea ahuweni ya haraka wale waliojeruhiwa,” wizara hiyo ilisema.

Mamlaka za Misri zinasema kuwa wamemkamata dereva wa gari anayeshukiwa kusababisha lori la mafuta kupinduka katika barabara kubwa ya mji wa Cairo, moto kuwaka na kuwaua watu wasiopungua 31 kipindi cha shughuli nyingi siku moja kabla.

Video ya shirika la AP ilionesha kuwa eneo hilo bado lilikuwa na masizi na moto uliotanda katika wingu la barabara inayounganisha jiji la Cairo na majimbo jirani ya Giza na Qalubiya Jumatano jioni.

Magari na wanaokwenda kwa miguu walikwama kwenye foleni kwa saa kadhaa kwenye barabara hiyo. Maafisa wa zimamoto walifanikiwa kuuzima moto na kuwatoa watu kwenye magari yaliyokuwa yamechomeka.

CHANZO:TRT Afrika and agencies