Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan atahudhuria mkutano wa pili wa kamati ya mkakati wa kisiasa na ulinzi ya Makubaliano ya ulinzi ya Makka jijini Islamabad siku ya Ijumaa, kulingana na vyanzo vya Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki.
Waziri wa Ulinzi Yasar Guler na Mkuu wa Majeshi Jenerali Selcuk Bayraktaroglu wataongozana naye.
Fidan anatarajiwa kusisitiza kuhusu dhamira ya Uturuki kwa makubaliano hayo ya ulinzi. Atasisitiza kuwa muungano huo ushughulikie changamoto katika kanda kupitia majadiliano, ushirikiano na umiliki.
Pia anatarajiwa kueleza umuhimu wa mashauriano na ushirikiano miongoni mwa wanachama kuhusu masuala ya usalama, na kusisitiza kuhusu dhamira ya Uturuki kwa amani, usalama na maendeleo katika kanda na zaidi. Waziri huyo pia atatathmini kuimarisha taasisi ya muungano.
Mashambulizi ya Houthi, mzozo wa Iran
Fidan anatarajiwa kulaani mashambulizi ya Houthi kwa raia na miundombinu yao, kuyataja yasiyokubalika na tishio kwa usalama na uthabiti katika kanda.
Atasisitiza kwa Uturuki kuwa pamoja na Saudi Arabia.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki pia atasisitiza umuhimu wa kuendeleza diplomasia kutatua matatizo kati ya Marekani, Israel na Iran, pamoja na kuhakikisha mipango ya wanachama ya kuhakikisha usalama baharini na matumizi salama ya Mlango Bahari wa Bab al Mandab.
Gaza, Ukingo wa Magharibi, Syria
Fidan anatarajiwa kueleza kuhusu hali mbaya ambayo Israel wamesababishia watu wa Gaza, kuendeleza makazi ya walowezi Ukingo wa Magharibi na ukiukwaji wa kihistoria katika eneo linalokaliwa la Jerusalem Mashariki.
Anatarajiwa kutoa wito kimsingi, wa maamuzi na hatua ya pamoja kimataifa kwa wanayofanya Israel, ambayo yanakiuka sheria ya kimataifa na maadili ya watu na kuendelea kutishia amani na usalama.
Waziri pia atasisitiza kuhusu msaada wa Uturuki kwa uhuru wa Syria, usalama wa kudumu na uthabiti katika nchi hiyo.
Kamati ya mkakati kisiasa na ulinzi
Rais wa Uturuki Erdogan, Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman walitia saini Makubaliano ya utatu ya Makka mwezi Agosti. Makubaliano hayo yanalenga kuimarisha usalama wa nchi hizo tatu kupitia juhudi za pamoja za kujilinda na ulinzi.
Majadiliano yanaendelea kuhusu kuimarisha taasisi ya muungano, ambayo msingi wake ni uhusiano wa muda mrefu kati ya Uturuki, Pakistan na Saudi Arabia.
Luteni Jenerali Mstaafu wa Pakistan Nauman Mahmood ameteuliwa kuwa katibu mkuu wa kwanza wa muungano huo. Sekretariati ikipangwa kuwa mjini Riyadh katika kipindi kifupi kijacho.
Kamati hiyo ilifanya mkutano wake wa kwanza jijini Istanbul mwezi Agosti, ikiangazia hatua zinazohitajika kutekeleza dira ya makubaliano ya kimkakati na kujenga taasisi imara ya muungano.
Ilikuwa na kikao chake mjini Riyadh tarehe 5 Oktoba baada ya mashambulizi ya Houthi kwa Saudi Arabia. Mataifa wanachama walisisitiza umoja wao na nia ya kulinda uhuru wa mipaka yao kwa mujibu wa makubaliano, kama ilivyoainishwa kwenye taarifa.














