Vikwazo vya Umoja wa Mataifa vimewekwa tena dhidi ya Iran kufuatia kushindwa kwa mazungumzo ya dakika za mwisho kuhusu mpango wa nyuklia, huku Ufaransa, Uingereza, na Ujerumani zikiionya Tehran dhidi ya "hatua za kuchochea."
"Kuwekwa tena kwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa si mwisho wa diplomasia," mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa matatu ya Ulaya, yanayojulikana kama E3, walisema katika taarifa ya pamoja Jumapili.
"Tunaisihi Iran kujiepusha na hatua zozote za kuchochea na kurejea kufuata majukumu yake ya kisheria yanayohusiana na usalama," waliongeza.
Kurejea kwa vikwazo dhidi ya Iran kulichochewa na mataifa hayo matatu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (Ujerumani kupitia mataifa mengine mawili) kutokana na madai kwamba nchi hiyo ilikiuka makubaliano ya mwaka 2015 yaliyolenga kuizuia kuunda bomu la nyuklia.
Iran inakanusha madai ya kutafuta silaha za nyuklia.