Sanae Takaichi, mwenye umri wa miaka 64 ni mhafidhina wa chama tawala cha Japan,Liberal Democratic Party (LDP), waziri mkuu wa kwanza mwanamke mwezi Oktoba, akishinda uchaguzi wa bunge na kufanikiwa ikiwa ni mara yake ya tatu kuwania nafasi hiyo.
Alikuwa upande wa waziri mkuu wa zamani Shinzo Abe, Takaichi ameahidi kufufua mkakati unaofahamika kama “Abenomics”, ambao unajumuisha matumizi makubwa ya umma na sera ya fedha yenye afuweni.
Muhula wa Takaichi unatoa fursa kwa Uturuki na Japan kufufua ushirikiano ambao haukufanikiwa wakati wa enzi za Abe.
Uwezo wa Japan wa sekta ya ulinzi unaoimarika na kupunguza masharti ya kuuza bidhaa nje ya nchi unakwenda sawa na kuimarika kwa sekta ya ulinzi ya Uturuki, kutengeneza fursa za maendeleo ya pamoja na kuimarisha uwezo wa kimkakati wa mataifa yote mawili.
Suala la kuwepo wa nishati ya kutosha ni eneo lingine la ushirikiano. Nafasi ya Uturuki kana kituo kikuu cha nishati katika kanda na dhamira ya Japan kuwa na vyanzo tofauti uya nishati, ikiwemo LNG ya Urusi, kunaweza kufanya kuwepo kwa majadiliano mahsusi ambayo yanaweza kusaidia katika siasa za nishati za mabara ya Ulaya na Asia.
Uhimili wa usambazaji, hasa kupitia Ushoroba wa Kati unaounganisha Uturuki na Asia Mashariki, unakwenda sanjari na juhudi za Japan kupata madini muhimu na kupunguza utegemezi kwa China, kuweka msingi wa ushirikiano katika masuala ya miundombinu na kuunganisha miradi kote Katikati mwa Asia.
Kwa misingi ya kidiplomasia, wote Takaichi na Erdogan wanakabiliana na hali za kisiasa wakiwa na uwezo mkubwa wa kimkakati, na kuziweka nchi zao kama zenye uwezo wa kuunganisha kanda na kusaidia katika upatanisho wa maslahi yanakinzana.
Kama serikali zote zitachukuwa fursa hii, ushirikiano mpya wa Uturuki na Japan wanaweza kuimarisha uwezo kutoka Mashariki mwa Mediterani hadi katika Bahari ya Hindi na Pasifiki, kuwa msingi muhimu wa enzi nyingine ya nchi zenye uwezo wa pande zote.
Siasa za nyumbani na Sanae Takaichi
Amezaliwa na kukuwa huko Nara na wazazi ambao hawakuwa wanasiasa, Takaichi alikuwa na maisha ya kawaida, akiwa mpiga ngoma, mtangazaji wa Televisheni,mpiga mbizi , na anayependa magari. Gari yake ya zamani ya Toyota Supra sasa iko kwenye makumbusho.
Ilikuwa wakati alipofanya na mbunge wa bunge la Congress Patricia Schroeder katika miaka 1980, wakati kukiwa na mvutano wa biashara kati ya Marekani na Japan, ambapo alianza kupenda siasa.
Hili likampa nafasi ya kuelewa kuwa Japan inahitaji uwezo wa kujitetea wenyewe badala ya kutegemea maoni ya Marekani.
Alichaguliwa bunge kwa mara ya kwanza 1993, akajiunga na chama cha LDP 1996 na kuwa mmoja ya wanachama wake wahafidhina wenye msimamo.
Alikuwa katika nafasi za juu mbali mbali, ikiwemo waziri wa usalama wa uchumi, biashara, na viwanda, na mambo ya ndani na mawasiliano.
Kufuatia majaribio yake ya kutafuta uongozi 2021 na 2024, alipta ushindi 2025. Wakati wa kampeni zake, aliwaambia watoto wa shule kuwa anataka kuwa ‘Iron Lady’ wa Japan, akifuata nyayo za Waziri Mkuu wa zamani Margaret Thatcher.
Ni mhafidhina ambaye anapinga wanawake walioolewa kuendelea kutumia majina yao ya mwisho ya kuzaliwa na kukataa ndoa za jinsia moja.
Amekuwa akitaka afuweni ya kodi kwa ajili ya uangalizi wa watoto, kusaidia huduma za kukaa na watoto na kuimarisha huduma kwa wanawake na wazee.
Mapendekezo haya yanatokana na aliyoyapitia wakati akihudumia jamaa zake.
Aliingia madarakani kipindi ambacho chama chake cha LDP kilikuwa kikikabiliwa na sakata mbali mbali, mdororo wa uchumi, kuwa na idadi kubwa ya wazee na ushindani kutoka kwa chama cha mrengo wa kulia cha Sanseito.
Kutokana na kupoteza wingi wake katika mabunge yote mawili na kukabiliwa na shutuma kutoka ndani ya chama, chama cha LDP sasa kinahitaji kupata wapiga kura na kujiweka kama mtetezi wa maslahi ya Japan.
Takaichi anasisitiza kuwa “LDP lazima ibadilike kwa lengo la sasa na mustakabali” na anajiona kuwa yeye ni mrithi wa siasa za itikadi za Shinzo Abe (1954–2022), kwa kuwa alieleza nia yake ya kumrithi.
Takaichi ameendeala na sera yake ya mambo ya nje ya kuimarisha ushirikiano ya kiusalama, kuongeza matumizi katika sekta ya ulinzi, na nafasi muhimu kwa jukumu la majeshi ya Japan.
Sera ambazo Abe aliziweka sawa, hasa kuhusu jukumu la Japan kuhusu kanda ya Bahari Hindi na Pasifiki, sasa ndiyo msingi wa dira ya Takaichi kuliko kuweka mipaka.
Muendelezo unaonekana wakati Japan inakabiliwa na vitisho kutoka nje ya nchi miungano ya kisiasa ndani ya nchi.
Uturuki, India, Indonesia, Afrika Kusini na Brazil wamejitambulisha kama wawezeshaji wakuu wa usalama na waratibu wa miungano ya kikanda.
Pia ni wadhamini wa shoroba mpya za uchumi na usalama.
Mataifa haya yanungana kwa lengo moja la uhuru wa kimkakati. Hata hivyo, wote pia wanakabiliwa na changamoto za pamoja za kuangalia ushirikiano wao na mataifa yenye uwezo mkubwa duniani bila ya wao kuonekana wanyonge kwao.
Japan itakuwa bora ikiwa ni nchi yenye uwezo wa kati, ikiangazia diplomasia ambayo haigemei Marekani au kanda baada ya Takaichi.
Kukataa kwake kusitisha kuagiza gesi ya LNG kutoka Urusi kunaonesha nia yake ya kutofautiana na Marekani pale inapohitajika, na mipango yake ya kuongeza matumizi ya sekta ya ulinzi inaonesha kuwa anataka kuwa na nafassi muhimu katika masuala ya usalama.
Makubaliano na Trump kuhusu madini muhimu kunaonesha juhudi za kubadili utegemezi wa kiuchumi kwa kuangalia maeneo mengine ya Bahari Hindi na Pasifiki.
Maamuzi ya Japan yanaendana na mabadiliko duniani miongoni mwa mataifa yenye uwezo wa kati kuhusu diplomasia, yakiongozwa na mtazamo wa Trump wa nipe nikupe, kuongezeka kwa uwezo wa China na walichojifunza kutoka kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Kwa hiyo Japan ya Takaichi inaonekana wakati ambao mtindo wa siasa za dunia za karne ya 20 zinafifia na miungano mengine inaibuka.
Kinachotokea nchini Japan ni sehemu ya miungano miongoni mwa mataifa yenye uwezo wa kati na siyo mambo yanayotokea ghafla.
Uturuki iko katikati ya ya Ulaya na Asia. Kwa upande mwingine, Japan, iko pembezoni mwa Pasifiki. Hata hivyo, shoroba za kimkakati zinazounganisha kanda hizo mbili, kutoka njia ya nishati za katikati mwaka Asia hadi katika njia za bahari, zinaendelea kuwa muhimu zaidi.
Katika muongo mmoja ujao, hayo mataifa yenye uwezo wa kati kote kwenye shoroba hizi kote katika shoroba hizi yatakuwa na umuhimu na ushawishi mkubwa.
Kwa muktadha huu mpana, Japan ya Takaichi inatoa nafasi ya fursa nyingine ya ushirikiano na Uturuki.
Wakati Uturuki ikiwa na mtazamo wa kuangazia sera ya mambo ya nje ya kuimarisha ushirikiano na mataifa mbali mbali, kuweka sawa uhusiano wake na NATO, Urusi, mataifa ya Ghuba, na Asia, Japan inaonekana kama mwenzake katika hili, wakati pia ikitaka kupanua wigo wa washirika wake.
Ushirikiano huu unatoa njia ya uhusiano zaidi wa kimkakati.



















