UTURUKI
2 dk kusoma
Hamas haina nuyklia, Israel iko nayo: Erdogan aitaka Berlin ichukue hatua kali dhidi ya Tel Aviv
Erdogan asema Uturuki na Ujerumani zinaweza kushirikiana kuhakikisha kupatikana kwa amani Gaza.
Hamas haina nuyklia, Israel iko nayo: Erdogan aitaka Berlin ichukue hatua kali dhidi ya Tel Aviv
Rais Erdogan wa Uturuki alaani mashambulizi ya hivi majuzi ya Israel dhidi ya Gaza. /
30 Oktoba 2025

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ambaye alikuwa mwenyeji wa Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz, jijini Ankara, Uturuki, amesisitiza kuwa Uturuki na Ujerumani zinaweza kuchukua nafasi muhimu kwa kushirikiana kumaliza vita vya Israel Gaza.

Akiwa pamoja na Merz baada ya mkutano wao Alhamisi, Erdogan alikosoa mashambulio ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya Gaza na kuitaka Ujerumani kuchukua msimamo mkali zaidi. 

“Hamas haina mabomu au silaha za nyuklia, lakini Israel iko nazo, na waliyatumia kuipiga Gaza jana,” Erdogan alisema. “Kama Ujerumani, hamuoni hili?”

Erdogan alisema Uturuki na Ujerumani, kama mataifa mawili yenye ushawishi mkubwa kikanda na kimataifa, wanaweza kushirikiana kuhakikisha amani Gaza.

“Uturuki na Ujerumani ni mataifa mawili muhimu ambayo yanaweza kushirikiana kumaliza vita Gaza,” alisema.

Erdogan aliwahimiza mashirika ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na Msalaba Mwekundu wa Ujerumani na Hila Nyekundu ya Uturuki, kuchukua hatua za dharura kukabiliana na mauaji ya halaiki na njaa katika ukanda wa Gaza.

“Msalaba Mwekundu wa Ujerumani na Hila Nyekundu ya Uturuki lazima zichukue hatua kuzuia mauaji ya halaiki na njaa huko Gaza,” alisema.

Kauli za Erdogan zilitolewa baada ya Israel kuwaua Wapalestina zaidi ya 100, wakiwemo watoto 46, huko Gaza tangu Jumanne jioni, na kukuika makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyokuwa yameanza tangu Oktoba 10.

CHANZO:AA