| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Raia wa Nigeria wametakiwa kurudisha mabaki kutoka mashambulizi ya anga ya Marekani
Kanda za mtandaoni zilionyesha wenyeji wakifukua vifusi na silaha zisizolipuka kwenye maeneo ya shambulio katika jimbo la Sokoto, na hivyo kuzua hofu ya milipuko mibaya.
Raia wa Nigeria wametakiwa kurudisha mabaki kutoka mashambulizi ya anga ya Marekani
Wakaazi wakikagua uharibifu baada ya wanajeshi wa Marekani kufanya mashambulizi dhidi ya magaidi wa Daesh nchini Nigeria. / Reuters / Reuters
3 Januari 2026

Jeshi la Nigeria liliwahimiza raia katika kaskazini magharibi mwa nchi siku ya Ijumaa wasiwe wanahifadhi au kugusa mabomu yaliyokosa kulipuka yaliyopatikana katika maeneo yaliyolengwa katika mashambulizi ya anga yaliyoongozwa na na Marekani hivi karibuni.

Tangazo hilo lilitokana na video zilizochapishwa mtandaoni zikionyesha wakazi wakichimbua mabaki na mabomu yasiyoripuka katika maeneo ya mashambulio jimboni Sokoto, jambo lililosababisha hofu ya milipuko hatari.

"Hatutarajii raia kuchukua au kuhifadhi vifaa kama hivyo," Meja Jenerali Michael Onoja, mkurugenzi wa Operesheni ya Vyombo vya Habari vya Ulinzi, aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa.

"Tunaweza tu kuwaomba warudishe vifaa vyote ambavyo vinaweza kuwa na madhara kwao."

Vikosi vya Marekani vilianzisha mashambulizi ndani kabisa ya Nigeria mnamo Desemba 25 kwa ombi la serikali ya Nigeria, kurusha mabomu 16 yanayoongozwa na GPS kutoka kwa ndege zisizo na rubani za MQ-9 Reaper kwenye kambi mbili zenye uhusiano na Daesh huko Sokoto.

Onoja alisema vitengo maalum vya askari ndani ya jeshi vilipewa jukumu la kutafuta vifusi na mabaki mengine kutoka kwa shambulio hilo.

CHANZO:Reuters