UTURUKI
1 dk kusoma
Erdogan: Uturuki kuharakisha miradi ya kiulinzi kuimarisha ‘maslahi’ na washirika wa Ulaya
Kulingana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, Ankara haipo tayari kuona ugaidi kwenye eneo lake wala kwa majirani zake.
Erdogan: Uturuki kuharakisha miradi ya kiulinzi kuimarisha ‘maslahi’ na washirika wa Ulaya
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan./Picha:AA
3 Novemba 2025

Uturuki itaendelea kuimarisha miradi yake ya kiulinzi na maslahi na washirika wake wa Ulaya, Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amesema.

"Wakati tukiweka kipaumbele kwenye miradi yetu ya kiulinzi, tutaendelea kuongeza ushirikiano na washirika wetu wa Ulaya kwa maslahi ya pande zote," alisema Erdogan wakati wa mkutano na wanahabari siku ya Jumatatu mara baada ya kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri jijini Ankara.

Akianisha baadhi ya miradi hiyo kama vile ule wa ndege za kivita maarufu kama KAAN, Erdogan aliweka wazi kuwa ndege hizo zitakuwa sehemu ya “Jeshi la Anga la Uturuki”.

"Kama vile HURJET inavyolenga kuongoza Nyanja hiyo, ndivyo tutakavyofanya kwa KAAN," alisema Rais Erdogan.

Erdogan alisisitiza kuwa Uturuki haitaki kuona aina yoyote ya ugaidi ikitamalaki katika eneo lake na nchi jirani, akisisitiza msimamo wa Uturuki wa muda mrefu wa kupambana na ugaidi.