| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
“Nyinyi ndio mustakabali”: Erdogan azindua chaneli ya vijana TRT Genc
TRT Genc itarusha vipindi mbalimbali vinavyolenga kusaidia ukakamavu wa kiakili, kihisia na kitamaduni kwa watazamaji vijana, anasema Rais wa Uturuki Erdogan.
“Nyinyi ndio mustakabali”: Erdogan azindua chaneli ya vijana TRT Genc
Rais Erdogan alitoa pongezi zake kwa wafanyakazi wa TRT na kuitakia chaneli mpya mafanikio. / / AA
tokea masaa 13

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amehudhuria Hafla ya Uzinduzi wa Chaneli ya TRT Genc, ikiashiria kuanzishwa kwa kituo kipya cha televisheni kinacholenga watazamaji vijana.

Akizungumza na vijana, wawakilishi wa vyombo vya habari na wageni katika Ukumbi wa Mikutano na Utamaduni wa Bestepe Millet siku ya Alhamisi, Erdogan alisema alifurahi kuwakaribisha vijana “katika nyumba ya taifa”, akiwataja kama mustakabali wa Uturuki.

Aliwapongeza wafanyakazi wa TRT na kukitakia kituo kipya mafanikio, akisema kitawanufaisha vijana, familia, sekta ya vyombo vya habari na taifa kwa ujumla.

Erdogan alisema TRT Genc itarusha vipindi mbalimbali vinavyohusisha sayansi na teknolojia, utamaduni na sanaa, michezo, historia na masuala ya sasa, kwa lengo la kusaidia ukakamavu wa kiakili, kihisia na kitamaduni ya vijana wanaotazama.

Alisisitiza umuhimu wa majukwaa kama hayo katika kukabiliana na kile alichokiita “janga la uraibu”, akibainisha ongezeko kubwa la utegemezi wa kutazama skrini, kamari za mtandaoni, na matumizi ya dawa za kulevya.

Mapambano ya kueleza “ukweli” yataendelea

Akionya kuwa familia imekuwa mojawapo ya uwanja mkuu wa mapambano ya kisasa ya “vita vya kitamaduni”, rais alisema taasisi ya familia iko chini ya shinikizo kubwa kuliko wakati mwingine wowote. Alieleza kuwa michezo ya kidijitali, ambayo huanza kama burudani, inaweza kuwa mtego unaowavuta vijana kuingia kwenye kamari ya mtandaoni.

Akitoa wito wa kuchukua hatua madhubuti zaidi kuliko matangazo ya huduma kwa umma pekee, Erdogan alisema Uturuki inapaswa kuchunguza tatizo la uraibu kwa undani zaidi na kulikabili kwa azma.

Aliongeza kuwa mapambano ya kueleza “ukweli” yataendelea katika nyanja zote kupitia taasisi mbalimbali, zikiwemo Shirika la Habari la Anadolu na Kurugenzi ya Mawasiliano.

Kuelimisha na kiburudisha vijana

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TRT, Mehmet Zahid Sobaci, alisema TRT Genc iliundwa kwa ajili ya vijana wanaojihisi kukwama kati ya maudhui ya watoto na vipindi vya watu wazima, na ambao hawakuweza kupata kituo safi, chenye ubora na kinachowalenga moja kwa moja.

Alisema kituo hicho kitajengwa juu ya dhamana ya serikali, maadili ya kitaifa na urithi wa kitamaduni.

Sobaci aliongeza kuwa TRT Genc pia kitawavutia wazazi, kwa kutoa mazingira salama ambapo familia zinaweza kutazama pamoja, kujifunza pamoja na kuimarisha mshikamano wao.

Alisema sifa kuu ya kituo hicho itakuwa uwezo wake wa kuelimisha huku kikiburudisha vijana kupitia watu wenye maarifa na ubora wa hali ya juu wanaoonekana kwenye skrini.

“Kwa kuonesha mawazo ya wajasiriamali vijana, miradi ya wavumbuzi vijana, na mikutano na wanaanga na wanasayansi wetu, tutawasilisha mifano bora kwa vijana wetu na kuwajengea hisia ya ‘mimi pia ninaweza,” alisema.

CHANZO:TRT World