Kwa kundi la AFC/M23 siku ya Alhamisi kudhibiti eneo la Uvira kwenye mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi kumesababisha hali wasiwasi kwa Jumuiya ya Kikanda ya Maziwa Makuu (ICGLR).
Akizungumza katika kikao maalum cha wataalamu wa masuala ya Ulinzi katika mji wa kitalii wa Zambia, Livingstone, naibu katibu mkuu wa Jumuiya hiyo, Yasir Mohammed, alisema mapigano yamesababisha madhila makubwa kwa watu, watu kuondoka katika makazi yao, na kutatiza shughuli za maisha.
Alitoa wito kwa nchi wanachama “kuchukua hatua madhubuti kuepusha kuongezeka kwa mapigano ambayo yamesababisha madhila kwa watu na kuwa hatari kwa usalama katika mataifa jirani," Paul Shalala, afisa uhusiano mwema wa Wizara ya Ulinzi ya Zambia, katika taarifa kwa waandishi wa habari.
Mkutano huo ulikuwa wa utanguliz wa ule wa wakuu wa majeshi wa ICGLR wenye lengo wala kujadili matatizo ya kikanda yanayosababishwa na mgogoro wa mashariki mwa Congo.
Shalala alisema Kamanda wa Jeshi la Zambia Geoffrey Zyeele alisema hali mashariki mwa Congo bado ni tete na inahitaji kushughulikiwa ili kulinda wanawake na watoto waliojikuta katikati ya vita.
Waliokutana mjini Livingstone ni wawakilishi kutoka mataifa 12 wanachama wa ICGLR -- Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Congo, DRC, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania, Uganda na Zambia.


















