Ulikuwa usiku mwema kwa Nigeria waliofungua kampeni yao ya ubingwa wa Afrika kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Tanzania.
Japo Walishinda, Nigeria walitolewa kijasho na Taifa Stars waliowabana unyo kwa unyo karibia mechi nzima, ishara kuwa Watanzania walikuja kazi sio mchezo.
Super Eagles walikuwa wamedhibiti sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza na walizawadiwa dakika tisa kabla ya kipindi cha pili wakati Semi Ajayi aliporuka juu zaidi na kufunga mpira wa kichwa uliopigwa na Alex Iwobi.
Kona ilipatikana muda mchache baadaye kufuatia beki wa Tanzania Bakari Mwamnyeto kuondoa hatari langoni kutoka kwa Victor Osimhen nje ya mstari.
Bao hilo liliakisi mamlaka inayokua ya Nigeria, huku Osimhen, Lookman na Moses Simon wakinyoosha safu ya nyuma ya Tanzania kupitia kasi na mwendo. Licha ya ubabe huo, Super Eagles hawakuweza kuendeleza uongozi wao kabla ya mapumziko wakisalia na uongozi wa bao moja pekee.
Taifa Stars waokolewa na VAR
Nusu ya pili ilianza kwa kishidni kutoka timu zote mbili. Nigeria walidhani walikuwa wameongeza uongozi wao kwa bao la pili dakika ya kwanza ya mchezo wakati Osimhen aliposukuma kisigino lakini bao hilo lilikataliwa baada ya ukaguzi wa VAR.
Tanzania ilishika kasi hiyo muda mfupi baadaye. Pasi yenye uzani mzito kutoka kwa Novatus Dismas ilitawanya ulinzi wa Nigeria , na kumruhusu Charles M’Mbowa kupenya na kuteremsha mchezo wa kumalizia na kupagawisha kipa Stanley Nwabali na kusawazisha mechi 1-1.
"Nadhani Tanzania ilicheza vizuri zaidi kuliko watu wengi walivyotarajia,’’ alisema kocha wa Tanzania Miguel Ángel Gamondi. ‘‘Nigeria walidhibiti mpira zaidi, lakini tuliwatawanya vyema kupitia mfumo wetu wa kimkakati. Walitengeneza nafasi, lakini nyingi zilitokana na ubora wa mtu binafsi - ambayo haishangazi. Kwa ujumla, naamini tuliwashangaza watu wengi kwa ubora wa mchezo wetu dhidi ya Nigeria leo." aliongeza kocha Gamondi.
lakini Nigeria ilizima mara moja imani yoyote ambayo Tanzania ilikuwa nayo ya kushikilia uongozi wa mechi. Ndani ya sekunde sitini, Lookman alitoa funzo kali, akidhibiti mpira kutoka kwenye ukingo wa eneo ambalo kipa hakuweza kufikia ili kurejesha uongozi wa Nigeria na kunyamazisha mbwembwe za Tanzania.
"Tumeridhika na pointi tatu,’’ alisema kocha wa Nigeria Eric Chelle. ‘‘ Hilo ndilo la muhimu zaidi. Kwa sasa, nataka kuzingatia mazuri. Sehemu ya pili ya mchezo inaonyesha wazi kwamba bado kuna kazi ya kufanya - hasa linapokuja suala la kuzima mechi. Tunafahamu hili, na tutalifanyia kazi.’’
Tanzania imesalia na mechi mbili za kundi lao C, ambapo watakutana na majirani Uganda Jumamosi usiku na kisha Tunisia Jumanne wiki ijayo.

