23 Desemba 2025
Mashabiki wa soka kutoka Tanzania wanaohudhuria michuano ya AFCON 2025 inayoendelea nchini Morocco, wamejinasibu kuwa timu yao ya taifa, maarufu kama ‘Taifa Stars’ itarejea na kombe, huku ikitupa karata yake ya kwanza dhidi ya Nigeria, Disemba 23, 2025.Mchezo huo utaanza saa mbili na nusu usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

