9 Septemba 2025
Mpaka sasa chama cha upinzania nchini Tanzania ACT Wazalendo hakijajua hatma ya mgombea wake wa urais Luhaga Mpina iwapo mahakama itamuidhinisha kuendelea kupeperusha bendera ya chama hicho.
Hii ni baada ya uteuzi wake kuingia dosari pale Monalisa Joseph Ndala, ofisa wa ACT-Wazalendo, alipowasilisha malalamiko akidai Mpina alikiuka kanuni za chama—hasa kwa kujiunga na chama akiwa amechelewa kwa hiyo hastahili uteuzi wa kugombea Urais.
Hata hivyo, jina lake la mwanasiasa huyo tayari limeingia katika historia ya siasa za Tanzania.