4 Septemba 2025
Aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Luhaga Mpina amesema hana mpango wowote wa kurejea kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza Septemba 3, jijini Dar es Salaam, Mpina ambaye uteuzi wake wa kugombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo ulitenguliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo (INEC), amesema kuwa hana mpango wa kurudi ‘nyumbani’, licha ya ombi lililotolewa na mgombea Urais wa CCM, Emmanuel Nchimbi.