2 Septemba 2025
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) nchini Tanzania kimezindua rasmi kampeni zake kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Katika moja ya ahadi zake, chama hicho kimeahidi kuongeza furaha miongoni mwa Watanzania, kwa kupunguza ukosefu wa ajira, na kufufua sekta za kiuchumi kama pamba na viwanda.