Ikiwa na utajiri wa rasilimali za samaki, Msumbiji imekuwa ikishuhudia matukio ya vimbunga./Picha: Reuters

Watu zaidi ya 90 wanahofiwa kufa maji baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya kaskazini ya Msumbiji, mamlaka za nchi hiyo zimesema siku ya Jumapili.

Chombo hicho, kinachokadiriwa kubeba takriban abiria 130, kilikutana na dhoruba hiyo kabla ya kufika katika pwani ya Jimbo la Nampula.

"Boti hiyo ilikuwa imejaa sana na ndio maana ikazama. Kuna watu 91 waliopoteza maisha katika ajali hiyo," Jaime Neto, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jimbo la Nampula amesema.

Kulingana na Neto, wengi waliokufa kwenye tukio hilo ni watoto.

Hofu ya Kipindupindu

Waokoaji wamefanikiwa kupata manusura watano katika tukio hili, hata hivyo walikuwa wanakabiliana na hali mbaya baharani wakati wakijaribu kuokoa watu wengine.

Idadi kubwa ya abiria hao walikuwa wanaondoka katika eneo la bara la nchi hiyo kwa kufuatia hofu ya kuibuka kwa ugonjwa wa Kipindupindu, Neto amesema.

Nchi hiyo, ambayo iko upande wa kusini mwa bara la Afrika, limeripoti visa zaidi ya 15,000 ya magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji na vifo 32, kuanzia Oktoba, kulingana na Serikali ya Msumbiji.

Eneo la Nampula ndilo lililoathirika zaidi, likiwa na na theluthi ya visa vyote hivyo.

Manusura wa Ajali

Katika miezi ya hivi karibuni, jimbo hilo limeshuhudia idadi kubwa ya watu wanaojaribu kukimbia mashambulizi ya kijeshi katika eneo la karibu la Cabo Delgado.

Kulingana na Neto, timu ya uchunguzi imeanza mchakato wa kujua chanzo halisi cha ajali hiyo.

Manusura wawili wa ajali hiyo walikuwa wakipokea matibabu hospitalini, amesema ofisa huyo.

Chombo hicho kilikuwa kinaelekea katika kisiwa cha Mozambique, ambayo ndio ilikuwa makao makuu ya koloni hilo la zamani la Ureno.

Kukabiliwa na Vimbunga

Eneo hilo la biashara ilitumika kama njia ya kuelekea India na wafanyabiashara Waarabu, liligunduliwa na mvumbuzi maarufu kutoka Ureno, Vasco da Gama.

Eneo hilo limeorodheshwa kama sehemu ya urithi wa dunia na Shirika la Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO).

Nchi hiyo imekumbwa na matukio ya vimbunga vya mara kwa mara.

TRT Afrika