Kulingana na vyombo vya habari, Waziri Mkuu huyo alikuwa anaelekea katika eneo la makazi la Baganis kwenye mpaka na Azerbaijan./Picha: Reuters      

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan amesema siku ya Jumamosi kuwa helikopta yake ilitua kwa dharura kutokana na uwepo wa hali mbaya ya hewa.

Tukio hilo limetokea karibu na Vanadzor, mji wa tatu kwa ukubwa nchini humo na mji mkuu wa jimbo la Lori, aliandika Pashinyan kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Սիրելիներս, ամեն ինչ կարգին է։ Եղանակային վատ պայմանների պատճառով մեր ուղղաթիռը չնախատեսված վայրէջք է կատարել Վանաձորում։ Այժմ ճանապարհը շարունակում ենք ավտոմեքենայով։ Լավ օր եմ մաղթում բոլորիս։

Posted by Nikol Pashinyan / Նիկոլ Փաշինյան on Saturday, May 25, 2024

"Imebidi helikopta yetu itue kwa dharura katika eneo la Vanadzor kutokana na hali mbaya ya hewa.

Kwa sasa, tunaendelea na safari yetu kwa gari. Nawatika siku njema," alisema.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, waziri mkuu alikuwa akielekea kwenye makazi ya Baganis kwenye mpaka na Azerbaijan, ambapo mpaka huo uliwekwa hivi karibuni.

TRT Afrika