#GHC21 : Tanzania kicks off campaign as Magufuli vies for new term / Photo: AFP

Leo ni siku ambayo waislamu kote Duniani wanaanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Lakini gharama za chakula lakini pia upatikanaji wake umekuwa mtihani katika baadhi ya maeneo.

Visiwani zanzibar hali ya hofu ya gharama za chakula imepelekea idadi kubwa ya watu kukusanya chakula kwa wingi ili kupunguza makali ya gharama ambazo zinahofiwa huwenda zikapanda zaidi siku chache zijazo.

Hali hiyo imepelekea Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi kutoa ufafanuzi kuwa chakula kipo na hakuta kuwa na uhaba wa chakula visiwani humo.

"Serikali imejiridhisha chakula kipo katika maghala mbalimbali ya wafanyabiashara wakubwa wanaoingiza chakula Zanzibar, hakunahaja ya wananchi kuwa na hofu ya upatikanaji wa chakula" anasema Hussein Mwinyi.

Hata hivyo Rais mwinyi amekemea wafanya biashara ambao wamenunua chakula na kuficha kwenye maghala yao wakisubiri kuongeza bei.

"Wito wangu kwa wafanyabiashara, wauze chakula kwa bei elekezi ya serikali na waache kuficha chakula kitendo hiki hakita vumiliwa" amesisitiza Rais wa Zanzibar

Mfumuko wa bei ya chakula bado ni tatizo Tanzania na na nchi zingine mbalimbali barani Afrika. Kwa mfano Kenya upatika naji wa Unga wa ugali bado ni changamoto kwani gharama ipo juu.

TRT Afrika