| Swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
Israeli yaharibu makazi 300 huko Jabalia mapigano yakiendelea Rafah
Israeli imeua watu 35,386, wengi wakiwa ni wanawake na watoto na kujeruhi zaidi ya 79,336, huku mashambulizi yake dhidi ya Gaza yakiingia siku ya 225.
Israeli yaharibu makazi 300 huko Jabalia mapigano yakiendelea Rafah
  “Mashambulizi ya Israeli yameua watu 83 na kujeruhi wengine 105 ndani ya saa 24,” Wizara ya Afya imesema./ Picha: Reuters   / Others

Idara ya Huduma za Ulinzi ya Palestina imesema kuwa majeshi ya Israeli yameharibu zaidi ya makazi 300 huko Jabalia kaskazini mwa Gaza, huku mapigano makubwa yakiendelea kughubika jiji la Rafah.

Msemaji wa idara hiyo Mahmoud Basal ameliambia shirika la Habari la Anadolu kuwa "majeshi ya Israeli yameharibu kabisa zaidi ya makazi 300 huko Jabalia toka kuanza kwa uvamizi wake.”

"Tunapokea taarifa nyingi za uwepo wa miili mingi barabarani na mingine ikiwa kwenye vifusi vya nyumba hizo," alisema huku akiongeza kuwa “vikosi vya uokoaji vinashindwa kufika eneo hilo kutokana na uzito wa mashambulizi ya majeshi ya Israeli."

Basal alieleza kuwa mashambulizi ya Israeli yamesababisha uharibifu mkubwa kwenye maeneo ya makazi katika mji wa Jabalia.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika