Meli hiyo ya mizigo ilikuwa imesajiliwa nchini Tanzania./Picha: Wengine

Timu ya waokoaji nchini Romania inaendelea na juhudi za kuwatafuta wafanyakazi watatu wa meli ya mizigo iliyozama katika pwani ya Bahari Nyeusi, Mei 18, 2024.

Meli hiyo ya mizigo iliyopewa jina la Mohammed Z, ilikuwa imesheheni bidhaa za ngano na mafuta kabla ya kuzama karibu na pwani ya Bahari Nyeusi.

Mapema Jumamosi, maofisa wa nchi hiyo walipata taarifa ya kuzama wa meli hiyo, kilomita 48 kutoka kijiji cha Danube nchini Romania.

Hadi inazama, meli ya Mohammed Z ilikuwa na wafanyakazi 11 ndani yake, tisa wakowa kutoka Syria wakati wawili walikuwa ni wamisri.

“Nane kati yao waliokolewa na meli ya abiria ambayo ilipita karibu yao," imesema taarifa iliyotolewa na kituo cha uratibu wa majini cha MRCC.

Meli ya mizigo ya Mohammed-Z ilitengenezwa mwaka 1988 na inapeperusha bendera ya Tanzania ikiwa imesajiliwa nchini Tanzania.

Bahari Nyeusi ni maarufu kwa meli za mizigo ya ngano na mafuta, huku ikitumika kwa pamoja na nchi za Bulgaria, Romania, Georgia, Uturuki, Ukraine na Urusi.

TRT Afrika