| Swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
Mkuu wa tume ya AU aelezea matumaini ya uchaguzi wa Senegal hivi karibuni
Hatua ya dakika ya mwisho ya Rais Sall kuahirisha uchaguzi wa Februari 25 ilisababisha mgogoro mbaya zaidi nchini Senegal katika miongo kadhaa
Mkuu wa tume ya AU aelezea matumaini ya uchaguzi wa Senegal hivi karibuni
Mkuu wa tume ya Umoja wa Afrika AU, Moussa Faki Mahamat akiwa Addis Ababa / Picha: Reuters / Reuters
18 Februari 2024

Mkuu wa tume ta Umoja wa Afrika AU ameelezea wasiwasi wake siku ya Jumamosi kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Senegal.

Hata hivyo, ameongeza kuwa anatumai uchaguzi "huru na wa uwazi" utafanyika nchini humo hivi karibuni.

Kauli za Moussa Faki Mahamat zimejiri katika kikao cha ufunguzi wa kongamano hilo la AU baada ya Rais wa Senegal Macky Sall kuapa Ijumaa kuandaa uchaguzi wa rais "haraka iwezekanavyo".

Baraza la kikatiba liliingilia kati Alhamisi suala hilo, naye rais, chini ya shinikizo kubwa ndani na nje ya nchi, aliahidi kuandaa uchaguzi "haraka iwezekanavyo", bila kufafanua tarehe yoyote maalum.

Hatua ya dakika za mwisho ya Rais Sall kuahirisha uchaguzi wa Februari 25 ilisababisha mgogoro mbaya zaidi nchini Senegal kuwahi kushuhudiwa katika miongo kadhaa.

Sall, ambaye amekuwa madarakani nchini humo tangu 2012, alisema kuwa alifuta uchaguzi huo kwa sababu ya mabishano kuhusu kutostahiki kwa wagombea na wasiwasi kuhusu kurejea kwa machafuko yaliyoshuhudiwa 2021 na 2023.

CHANZO:AFP