Moja ya kazi za  Hassouna./Picha: AA

Mustafa Hassouna, mpiga picha kutoka Shirika la habari la Anadolu, amepokea "Tuzo Maalum" katika shindano la picha la kimataifa la WPP kutokana na kazi yake inayoangazia mashambulizi ya "Israeli dhidi ya Gaza."

Tuzo hiyo ilitolewa siku ya Ijumaa na mwana wa Mfalme Constantijn wa Uholanzi katika sherehe zilizofanyika Amsterdam.

Mashindano hayo yaliangazia picha zinazoonyesha uharibifu na maafa ya kibinadamu katika eneo la Gaza la Palestina ambalo limeandamwa na mashambulizi ya Israeli.

Mwaka 2018, Hassouna alishiriki tuzo za Shirika la habari la Guardian na mwaka 2014, shirika hilo lilichagua kazi yake kama moja ya kazi bora duniani.

Tuzo hiyo inakuwa ya pili kutwaliwa na shirika la habari la Anadolu mpaka leo.

Shidano hilo huandaliwa na taasisi ya kiholanzi ya wapiga picha ikisaidiwa na familia ya kifalme ya Uholanzi.

Picha za Shirika la Anadolu hapo awali zimewasilishwa kama ushahidi kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), ambayo imeishutumu Israel kwa kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Shirika la habari la Uturuki pia limekusanya picha hizo katika kitabu kiitwacho "Ushahidi" kitakachotumika katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) huko The Hague.

Kesi ya ICC mjini the Hague

Miezi saba ya vita vya Israeli dhidi ya Gaza, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) wiki iliyopita imetoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant kwa uhalifu wao wa kivita dhidi ya Wapalestina.

Zaidi ya miezi saba ya vita vya Israeli, maeneo makubwa ya Gaza yamegeuka kuwa magofu huku kukiwa na kizuizi cha upatikanaji wa chakula, maji safi na dawa.

Israeli imeendeleza mashambulizi yake makali dhidi ya Gaza tangu Oktoba 7, 2023, licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano katika eneo hilo.

Takriban Wapalestina 35,800 wameuawa, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na zaidi ya wengine 80,200 kujeruhiwa tangu Oktoba mwaka jana.

TRT Afrika