| Swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
Msumbiji yapiga marufuku maandamano ya vyama vya upinzani
Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Pascoal Ronda amefananisha maandamano hayo na "vitendo vya kigaidi".
Msumbiji yapiga marufuku maandamano ya vyama vya upinzani
Maandamano nchini Msumbiji yaliitishwa na Venancio Mondlane kutoka chama cha upinzani./Picha: Reuters / Others
15 Novemba 2024

Mamlaka nchini Msumbiji zimepiga marufuku maandamano yanayoendelea nchini humo toka kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 9.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo, Pascoal Ronda alitoa tamko hilo siku ya Ijumaa, huku akiwataka raia wa nchi hiyo kushirikiana na mamlaka "kuzuia machafuko yanayotokana na maandamano hayo."

Akielezea maandamano hayo kama "vitendo vya kigaidi," Ronda alisema: Serikali haitoruhusu maandamano haya yaendelee kuivuruga nchi yetu.”

Maandamano makubwa yameikumba nchi hiyo, toka kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi siku ya Oktoba 24 ambayo yalimpa ushindi Daniel Chapo kutoka chama cha Frelimo kwa asilimia 70 za kura, huku Venancio Mondlane akipata asilimia 20.

Siku ya Oktoba 31, Mondlane aliitisha maandamano ya wiki nzima nchini humo, kwa nia ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo. Mamia ya watu wameitikia wito huo.

Waandishi wa habari wa nje wakamatwa

Waandishi wa habari wawili, Bongani Siziba na Sibonelo Mkhasibe, walikamatwa siku ya Jumatano wakati wakifuatilia maaandamano hayo jijini Maputo.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika